Maafisa wanaochunguza chanzo cha moto katika uwanja wa ndege wa - TopicsExpress



          

Maafisa wanaochunguza chanzo cha moto katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta Jumatano iliyopita hawafutilii mbali ugaidi au njama ya uhalifu, lakini pia wanasema huenda ilikuwa ajali tu. Jana uchunguzi huo ulipata msukumo wa kimataifa wakati maafisa watatu wa idara ya upelelezi ya Marekani, FBI, waliotumwa na ubalozi wa Marekani mjini Nairobi, walipojiunga na kikosi cha wachunguzi. Ilikuwa ni siku moja tu baada ya rais wa Marekani, Barack Obama, kuzungumza na rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, na kupendekeza msaada wa serikali yake baada ya moto huo. Unasemaje kuhusu Wamarekani kusaidia kutafuta chanzo cha moto huo?
Posted on: Fri, 09 Aug 2013 09:29:29 +0000

Trending Topics




© 2015