Marekani na waitifaki wake wa Magharibi hususan Uingereza na - TopicsExpress



          

Marekani na waitifaki wake wa Magharibi hususan Uingereza na Ufaransa pamoja na Uturuki, Saudi Arabia na Qatar zinadai kuwa zingependelea kuona mgogoro wa Syria ukimalizika. Hata hivyo wakati huo huo nchi hizo zinaendelea kuwapatia silaha, kuwafadhili kifedha na kutoa mafunzo kwa wapinzani wanaobeba silaha na makundi ya kigaidi yanayoipinga serikali ya Rais Bashar al Assad wa Syria. Hasa ikizingatiwa kuwa tangu kuanza machafuko huko Syria na kushadidi hali ya mgogoro nchini humo, nchi za Magharibi hasa Marekani, Uingereza na Ufaransa pamoja na waitifaki wao wa Kiarabu zimechukua stratejia ya kuisambaratisha serikali ya Damascus na kufanya hatua nyingi za uharibifu katika uwanja huo. Hatua hizo zinajumuisha kuwafadhili kifedha, kuwapa misaada ya kilojistiki, kijasusi na silaha kwa makundi ya upinzani ya Syria. Marekani imezidisha hatua hizo za uharibifu ikiwa ni pamoja na kuzidisha misaada yake ya silaha na mafumzo kwa wapinzani wa Syria ili kuipindua serikali ya nchi hiyo haraka iwezekanavyo. Hii ni katika hali ambayo Jay Carney, msemaji wa White House alisema hapo jana kuwa kuna udharura wa kubadilishwa mlingano wa nguvu kwa maslahi ya wapinzani na kusisitiza kwamba, serikali ya Marekani huwenda ikawapatia wapinzani wa Syria silaha nyepesi na makombora dhidi ya vifaru. Jay Carney ameyasema hayo baada ya Congresi ya Marekani kukubali kwa tahadhari mpango wa serikali ya Obama wa kutaka kuyatumia silaha makundi ya upinzani ya Syria. Carney amesema kuwa, kutumiwa silaha makundi ya upinzani kutawaandalia uwanja mzuri wa kuendeleza vita dhidi ya serikali ya Damascus na hatimaye kushinda. Pamoja na matamshi hayo yote, msemaji huyo wa ikulu ya Marekani hakuashiria vipi silaha hizo watakazotumiwa wapinzani huko Syria zitabadilisha kikamilifu hali ya mambo katika medani ya vita nchini humo na kuyapa ushindi makundi ya upinzani ambayo katika wiki zilizopita yalipata pigo kubwa kutoka kwa jeshi la Syria. Marekani hivi sasa ina majeshi huko Jordan na mbali na kikosi hicho ina ndege kadhaa aina ya F 16 na imeweka makombora ya patriot karibu na mipaka ya Jordan na Syria na kuna uwezekano ikatumia zana hizo za kijeshi ili kuasisi eneo lisiloruhusiwa kuruka ndege nchini Syria. Hii ni katika hali ambayo Jenerali Martin Dempsey, mkuu wa vikosi vya majeshi ya Marekani alitangaza siku kadhaa zilizopita kwamba jeshi la nchi hiyo limejiandaa kufanya oparesheni mbalimbali huko Syria katika fremu ya kuwaunga mkono wapinzani wa serikali ya Damascus iwapo White House itaomba kutekelezwa jambo hilo. Kwa mujibu wa matamshi ya huko nyuma ya Dempsey tunaweza kufikia natija kuwa, Marekani ina njia mbalimbali za kuingilia kijeshi huko Syria. Njia hizo ni pamoja na kuendesha mashambulizi ya kijeshi, kuanzisha eneo lisiloruhusiwa kuruka ndege, kuongeza misaada na vilevile kutoa mafunzo kwa wapinzani. kiswahili.irib.ir
Posted on: Wed, 24 Jul 2013 18:10:15 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015