Matangazo yatu ya kiswahili yapo hewani kukujuza yanayojiri - TopicsExpress



          

Matangazo yatu ya kiswahili yapo hewani kukujuza yanayojiri asubuhi hii, upo naye Sabina Nabigambo, ambapo miongoni mwa habari tunazo ni pamoja na: Uhasama wa kidiplomasia baina ya Kenya na Uingereza waendelea kuongezeka baada ya Kenya kuikashifu Uingereza kuwa ina mipango ya kuhujumu mapendekezo yake mbele ya kikao cha mataifa wanachama wa mahakama ya ICC, kesi ya wanajeshi zaidi ya arobaini nchini DRCongo wanaotuhumiwa makosa ya Ubakaji mjini Minova mwaka 2012, imeahirishwa hadi Desemba 4 mwaka hii. Watu kumi na tano wauawa katika mapigano ya kikabila yaliyotokana na mzozo wa kipande cha ardhi katika jimbo la Unity, nchini Sudan kusini Na Serikali ya Marekani yatangaza kukubaliana na Rais wa Afghanistan kuhusu uwepo wa majeshi ya Marekani baada ya vikosi vya NATO kuondoka nchini humo mwakani.
Posted on: Thu, 21 Nov 2013 04:43:55 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015