Msemaji Mkuu wa Serikali akanusha taarifa zilizoandikwa kwenye - TopicsExpress



          

Msemaji Mkuu wa Serikali akanusha taarifa zilizoandikwa kwenye mtandao wa “twitter ” na wanyarwanda kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ni shemeji wa aliyekuwa Rais wa Rwanda Juvenal Havyarimana. “Taarifa hizi haina ukweli wowote na zinalenga kumpaka matope Rais Jakaya Mrisho Kikwete,”amesema msemaji wa serikali na kufafanua kuwa lengo la mitandao ya kijamii ni kuhabarisha na kuelimisha umma wala siyo kupotosha jamii kwa kuandika habari zisizo na ukweli wowote. Madai hayo yaliandikwa jana na mitandao ya Rwanda wakidai kuwa mama Salma Kikwete ni Mnyarwanda na ni binamu wa aliyekuwa rais wa zamani wa Rwanda.
Posted on: Tue, 20 Aug 2013 15:21:06 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015