NIMEIKOPI TU,,NA KUEPESTI HAPA. KWA WALE NDUGU ZANGU - TopicsExpress



          

NIMEIKOPI TU,,NA KUEPESTI HAPA. KWA WALE NDUGU ZANGU WANAOMSHAMBULIA ZZK KUHUSU MAAMUZI YA PAC DHIDI YA RUZUKU KWA VYAMA 6 VYA SIASA !!! #AUDITING An unbiased examination and evaluation of the financial statements of an organization. It can be done internally (by employees of the organization) or externally (by an outside firm). Kwa kutumia maneno ya hapo juu kulingana na kauli ya Mheshimiwa ZZK kuwa vyama vya siasa 6 havijakaguliwa na CAG ni sawa kwani kutokana na sheria ambayo anasema imefanyiwa marekebisho na kumtaka CAG kupeleka wataalamu kufanya AUDITING katika vyama vya siasa haijawa implemented. Chadema kupitia Mr. Komu baada ya sakata kuanza aliibuka na kutoa kauli kama mtu muhusika akilalamika kuhusu hatua wanazotaka kuchukua PAC za kutoa maelekezo kwa Msajili wa vyama ili waache kutoa ruzuku kwa vyama hivyo sita mpaka pale matumizi ya #Ruzuku katika vyama hivyo yatakapotiwa. Mr. Komu alienda mabali akiomba CAG ndiye awe mkaguzi wa pesa hizo,....kitu ambacho kinaashiria kuwa ni kweli ofisi ya CAG haijawahi kupita katika vyama hivi. Mbali na vyama hivi kutoa matumizi yake in public kwamba wamepeleka taarifa zao za fedha ya #Ruzuku kwa msajiri baada ya kuzipitia wao kama vyama husika na watu wao ambao hatutegemei wapeleke taarifa zenye matatizo kwani tayari hao watu wana interest katika vyama vyao kwa maana ya kibarua. So haitatokea vyama hivi vishindwe kucheza karata ya kubumba mahesabu. Kupitia Mwenyekiti wa PAC ZZK na wajumbe wengine ,..ZZK amesema sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992 inayosema Section 18 (2) Subventions granted to a political party shall be accounted for to the Registrar, separately from the accounting for other funds of the party. Imebadilika baada ya yeye mwenyewe mwaka 2008, alipeleka pendekezo la mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa katika Bunge la Novemba kutaka vyama vikaguliwe na CAG, na pendekezo lake lilisomeka: “Vyama vyote vitakaguliwa na CAG na itakuwa ni jukumu la vyama vya siasa kupeleka taarifa zao kwa CAG kwa mujibu wa sheria.” Kutokana na maneno hayo hapo juu ni jukumu la CAG kuhakikisha vyama vyote vya siasa vinakaguliwa na si vinginevyo, kwani CAG naye ameingia katika malumbano na PAC akihoji kwamba ni lini Chadema wamepeleka hiyo report aikague ? Kwa maana nyingine Organization yeyote isipopeleka matumizi yake ya fedha za UMMA CAG hawajibiki? MY TAKE!!! 1.Watanzania tuache ushabiki ambao hauna maana kwani nia ya ZZK ni njema tuh kwa Taifa, na siku zote tumekuwa tukisema Taifa kwanza mambo mengine baadae. Kama sheria inamtaka CAG na office yake wafanye auditing ya ruzuku kwa vyama hivi inampasa atimize wajibu wake. 2.Tanzania inawahitaji wazalendo na si washabiki wa vyama, Taifa hili linahitaji wazalendo watakao iweka nchi mbele na si masilahi ya kikundi cha watu wachache ama masilahi yao, So tuwe waangalifu kwani tumekuwa tukilalamika kwa 50 yrs lakini taabu zetu na njaa zetu hazitufanyi kuwa critical thinker kwenye issues za msingi tunaanza ushabiki. 3.Tujifunze na tuwe na Tabia kuwapa nguvu watu wote wenye nia njema na nchi hii kwani haitakuja kutokea tukapata maendeleo kwa kuweka interest za magroup ya watu na ya kwetu huku tukiliweka Taifa rehani. Huo ni upuuzii !!! Lazima tukae pamoja tujadili maswala sensitive ya nchi hii na tuyapatie majawabu. 4.Leo hii tunapoteza muda mwingi tukijadili watu yaani tuko subjective and not objective when it comes to national matters which is something ridiculous for our country. Its high time to think abt wat are we fighting for and who is our real enemy? 5.Adui wa watanzania hata siku moja hawezi kuwa chama cha siasa ,adui yetu mkuu ni jinsi tunavyofikiria na kuwaza juu ya matatizo yetu kwamba ni jinsi gani tunatoka. CCM ,CHADEMA , CUF na wengine wote ni vyama vya siasa wote hawa wana interest zao za chama na Taifa. So we should be very careful otherwise we ar fighting a loosing battle. By the Citizen Kiberiti Emmanuel Jr
Posted on: Mon, 21 Oct 2013 19:16:03 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015