Naomba hili tulipe mtazamo mzito inavyostahili. Tuna mgogoro wa - TopicsExpress



          

Naomba hili tulipe mtazamo mzito inavyostahili. Tuna mgogoro wa mpaka na Malawi. Zambia salama.Tuna kutokuelewana na M23 wa DRC ikisemekana Al Shabab wanawaunga mkono! Burundi salama. Tuna maneno neno na Rwanda. Rwanda na Uganda (Kagame na Museveni) ni walewale. Sudan Kusini salama. Tuna vinyongo na Sudan. Tusidanganyane, kwa sasa usalama wetu uko mashakani hasa ukizingatia pia utajiri mkubwa wa madini tulio nao. Sudan wana chuki mno na Marekani kwani kama si miongoni mwa walioasisi suala la Al Bashir kushtakiwa ICC, basi wanaliunga mkonosulala hilo huku sisi tukiwa na urafiki na Marekani, maadui wa Sudan. Kenya hawako vizuri na Marekani kwa jinsi inavyowatenga kwa kumchagua kiongozi mwenye kesi ICC. Naamini ukaribu wetu na Marekani hauwafurahishi. Lazima watakuwa wametununia. Katika mpango wa kututenga wa Rwanda, Kenya na Uganda kuna suala la kusafirisha mafuta kwa bomba toka Sudan Kusini kwenda Uganda na Rwanda. Kwa maana hiyo, Sudan Kusini nao wamelazimishwa wawemo kwenye timu ya kututenga. Kama walivyo Rwanda, Watutsi wa kabila la Kagame wapo pia Burundi na wenzetu hawa wana viapo vibaya ukikosana na mtu wa kabila lao. Kwa msingi huo, majirani wetu salama watabaki kuwa Msumbiji, Zambia na Burundi lakini kwa Burundi, mtu mmoja mmoja watakuwa wanatuchukia pia. Katika hali hii, kwanza, ni vizuri tuifahamu hali hii tuliyo nayo. Pili, tusahau na kupuuza vuta nikuvute zetu za ndani za CCM kwa CCM kuhusu kuteuliwa ugombea wa urais 2015 (tunakokuita kwa makosa “urais 2015”),za CCM na CDM, CDM na CUF nk. SASA TUNAPASWA TUJENGE MSHIKAMANO IMARA WA KITAIFA NA TUWE KITU KIMOJA KABISA DHIDI YA HATARI ZOZOTE TOKA NJE. Sasa hivi si salama kabisa kujitangaza kwamba tuna magaidi miongoni mwetu ili usiwe mwanya kwa maadui zetu wa nje kutufanyia ugaidi wa kikweli. Tatu, sasa hivi vyombo vyetu vya usalama wa nchi kama Polisi, Uhamiaji na Taasisi ya Serikali ya utafutaji wa taarifa za kuhatarisha usalama wa nchi vinapaswa vijizatiti sana kutafuta taarifa za watu wanaojipenyeza na kuishi nchini mwetu kijanja. Mtazamo wa shughuli zetu kwa sasa uwe huko zaidi ili watu wa M23, Al Shabab na wengine wote wenye nia mbaya kwetu wasiwepo nchini kutuangamiza. Nne, sisi wananchi wote, hasa wa mahotelini, kwa sasa tuwe mashushushu wa kunusa nusa taarifa zote za watu wanaoweza kuhatarisha nchi yetu na tukipata mashaka yoyote ya msingi dhidi ya mtu yeyote yule, tumripoti mara moja bila kujali huenda atagundulika si mtu hatari. Naomba sana tujenge mshikamano wa kitaifa kukabili chochote cha hatari toka nje. Mungu ibariki Tanzania.
Posted on: Wed, 24 Jul 2013 00:58:44 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015