Nchini Tanzania ambako serikali ya nchi hiyo kupitia mwanasheria - TopicsExpress



          

Nchini Tanzania ambako serikali ya nchi hiyo kupitia mwanasheria wake mkuu jaji Fredrick Mwita iliiandikia barua mahakama ya uhalifu ICC kutaka makamo rais wa Kenya William Ruto kutohudhuria baadhi ya vikao vyake katika kesi inayomkabili ya uhalifu dhidi ya binaadamu katika ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007. Jaji Fredrick amesema ameandika barua hiyo ili Ruto aweze kutimiza majukumu yake kama kiongozi nyumbani nchini Kenya. Ombi kama hilo lililotolewa na wakili wa Ruto kwa mahakama ya ICC lilikataliwa na mwendesha mkuu Fatou Bensouda na sasa linasubiri hukumu ya majaji. Hata hivyo habari hii imekuwa gumzo nchini Tanzania huku baadhi ya raia huko wakisema hawaoni mafungamano ya kesi hiyo na Tanzania. Je, huu ndio mwanzo wa nchi za kiafrika kujitoa katika mkataba wa Roma?
Posted on: Thu, 12 Sep 2013 09:47:17 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015