"Ndugu Watanzania kwakweli kuna mambo ya kuyafumbia macho lakini - TopicsExpress



          

"Ndugu Watanzania kwakweli kuna mambo ya kuyafumbia macho lakini linapo fika suala linalokuja kuharibu sura ya Tanzania hasa hili tukio la kuwamwagia TINDIKALI watalii tena watalii wenyewe ni walimu waliokuja kujitolea kuwafundisha watanzania masomo ya sayansi ni aibu sana tena sana hasa kwa watu kama sisi ambao tunatembelea nchi za ulaya na marekani kila mwaka pia nia hatari sana kwa watanzania ambao wapo nchi mbalimbali. Kwann tumeweza kufikia hapa? why mtalii? kwasasa ukienda baadhi ya nchi kama ni mtanzania unavuliwa nguo zote mbali ya hapo unawekwa kwenye machine za mionzi kukuchunguza mpaka kwenye utumbo kama umebeba madawa..kwann tufikie huku? kwann watu wachache watuharibie sura yetu kama nchi? Miaka michache iliyopita watanzania hukiwa nchi za watu huko tulikuwa tunaheshimika hata kwa umaskini wetu hii ilitokana na image mzuri ya nchi yetu..tunavyo shughurikia matatizo ya nchi mbalimbali, majeshi yetu yapo nchi mbalimbali kwa kulinda amani under UN umbrella. TUKATAE hizi tabia..huwezi kujua athari ya hili tukio leo..lakini siku za usoni utakapo ishi mbali na nchi yako ndio utakuja kujua madhara ya hili tukio. Image ya TANZANIA imeharibika kwa mtu au watu fulani wajinga wanao fanya mambo kwa masilahi yao na siyo ya nchi" TUKATAE TABIA MBAYA NA ZA KIJINGA..KATAA KUTUMIWA Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Africa
Posted on: Sat, 10 Aug 2013 10:39:04 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015