Nimeicopy kama ilivyo, songa nayo:- HIVI TANZANIA BILA - TopicsExpress



          

Nimeicopy kama ilivyo, songa nayo:- HIVI TANZANIA BILA “USANII” HAIWEZEKANI..? Kweli sikio la kufa halisikii dawa labda ndio maana Rais Mwinyi alipoona hatufanikiwi kwenye mchezo wa soka alisema "Tanzania nikichwa cha mwenda wazimu" Leo gazeti la FAHAMU limeandika "CHEKA APEWA MKANDA FEKI" • Mkanda alioutwaa hautambuliki popote duniani • Bondia aliyepigana nae hajawahi kutwaa taji lolote duniani • Makanda wa Super midleweight aliokabidhiwa Cheka unashikiliwa na bondia wa Australia Sakio Bika na sio Phil Williams kama ilivyodaiwa. UCHUNGUZI Baada ya kusoma habari hiyo nikaamua kudadisi kwa kufuatilia kwenye mitandao mbalimbali ya habari duniani ikiwa ni pamoja na ENEWS, AFP, GOOGLE SEARCH, WIKIPEDIA etc. FINDINGS (Niliyoyagunduani haya): • Ni kweli Mkanda wa Super midleweight aliokabidhiwa Cheka unashikiliwa na bondia wa Australia Sakio Bika tangu mwaka 2008. Mwaka jana 2012 alitetea taji lake (la Super middle weight champion) kwa kumpiga Nikola Sjekloca. • Bondia aliyepigana na Cheka (Phil Williams) ni bondia lakini hakutambulika na Mashirikisho Rasmi ya ndondi duniani kama WBA, WBF,IBF etc . • Amewahi kucheza ndondi lakini hajatwaa ubingwa wowote wa dunia, anatambulika na chama cha ndoni jimboni kwao Minnesota Boxing Association. Amekuwa akicheza mapambano madogomadogo na kabla ya kuja Tanzania alicheza na Charles Goodwin katika ukumbi wa Seven Clans Casino. (Immagine mtu anayecheza kwenye viCassino analetwa Tanzania kama bondia maarufu). • Kazi rasmi ya Phill Williams anayoifanya na inayomtambulisha ni KINYOZI (Barber). Anamiliki saluni yake huko Minneapolis Marekani ambapo anajishughulisha na kunyoa nwele, kusuka, kukata kucha, kupaka rangi etc. Soma zaidi hapa en.wikipedia.org /wiki/ Phil_Williams_(b oxer). MY TAKE..!! Walioandaa pambano la Cheka na Phil Williams walituambia kuwa ni bingwa wa dunia wa uzito wa kati (Super Middle Weight Champion). Waandishi wa habari nao wakadakia na kumpa uzito mkubwa Williams bila kufanya uchunguzi, kumbe kinyozi. Hapa niwalaumu kidogo waandishi wenzangu wa Habari. Magazeti, Radio, TV, Blogs vyote vilipambwa na habari ya Cheka kuwa atapigana na Bingwa wa Middle weightduniani. Je hakuna hata mmoja aliyeweza kuchunguza na kubaini ukweli kabla bondia wetu Cheka hajapigana na huyo "mkata kucha" wa Minneapolis..? Niwapongeze waandishi wa gazeti la FAHAMUkwa kuibua hili lakini ingekuwa vema kama ingegundulika mapema zaidi ili pambano hilo lifutwe. Tumejidhalilisha kumruhusu bondia makini kama Cheka kupigana na Kinyozi. Hivi Cheka angemuulia jukwaani tungewaeleza nini vinyozi wenzie wa Minneapolis..?? Lakini kwanini Watanzania tufanywe wajinga kwa kuletewa kinyozi na kuambiwa ni bondiatena anayeshikilia mkanda wa dunia wa uzitowa juu duniani..??Nanialithubutu kufanya udanganyifu mkubwa hivi bila kuogopa? Promota wa pambano hili Jay Msangi amewezaje kuidanganya hadi serikali bila woga na kufikia hata kumualika waziri wa Habari Dkt. Fenella Mukangara? Tena nasikia alialikwa Rais Kikwete lakini kutokana na majukumu akamuagiza Dk.Mukangara amuwakilishe. Hii ina maana kuwa hata Rais Kikwete alidanganywa? Je huyu Promota Msangi ndio mwenye ujasiri wa kumdanganya hadi Rais au kuna watu nyuma yake? Na kama Rais Kikwete amedanganywa katika hili la kuletewa kinyozina kuambiwa ni bondia, je Rais wetu ameshadanganywamangapi? Na kama Rais anadanganywa, usalama wa taifa hili uko wapi? Hawa wanaomdanganya si wanaweza kutake advantage hiyo na kuihujumu nchi yetu? Usalama wa Taifa wanafanya kazi gani? Hivi hata katika hili la kuletewa Kinyozi na kudanganywa ni bondia, usalama wa taifa hawakuliona? Au wamecocentrate kwenye “kung’oa watu kucha na meno” na kusahau mambo yanayohatarishausalama wan chi?? Na ikiwa tunafanya usanii hadi kwenye mambo serious hivi na kuwadanganya Watanzania wote tutegemee maendeleao kwenye sekta ya michezo nchini? Shirikisho la ndondi Duniani WBC na IBO wanamtambua Sakio Bika (wa Australia) kuwa Bingwa wa uzito wa kati duniani, je saivi wakiambiwa kuna bondia Tanzania anaitwa Cheka nae anashikilia taji hilo haitatucost? Wanaweza kuifungia Tanzania kushiriki mashindano ya kimataifa kwa kufanya uhuni. Hivi kwanini usanii umekuwa ndio sifa ya watanzania? Nashauri promota aliyeandaa pambano lile Jay Msangi akamatwe na kushitakiwa kwa uhuni huu. Ashtakiwe kwa kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, ashatakiwe kwa kumdanganya Rais, na kwa kuhatarisha maisha ya kinyozi wa Marekani. HIVI TANZANIA BILA USANII HAIWEZEKANI..??
Posted on: Tue, 03 Sep 2013 13:13:25 +0000

Trending Topics



>
Seeking Good Companions - Description: The value of good friends.
Here is a list of the current Self-Employment Trainings around
DONT JUST START A BUSINESS, SOLVE A PROBLEM Yes, folks.

Recently Viewed Topics




© 2015