RIWAYA : MISS TANZANIA SEHEMU YA 14 ILIPOISHIA SEHEMU - TopicsExpress



          

RIWAYA : MISS TANZANIA SEHEMU YA 14 ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA “Naitwa Happy ..Happy Kibaho ,natokea Tanzania” “Uuugh ! nafurahi sana kusikia unatoka Tanzania.I love Tanzanians.Nasikia ni watu wapole na wakarimu sana.Mama yangu amewahi kwenda Tanzania kupanda mlima Kilimanjaro na aliporudi akatuhadithia kuwa hajawahi kukutana na watu wakarimu kama watanzania.” Happy akatabasamu .Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Michelle kumuona happy akitabasamu. “Happy you are so pretty.Unajua sikuwahi kukuangalia vizuri.You are amazing” Michelle akajibu na kumfanya Happy afurahi. “Jina lako zuri sawa kabisa na sura yako..ukitabasamu unakuwa mzuri zaidi ya malaika..” akasema Michelle na kumfanya Happy acheke kwa nguvu. Huo ukawa ni mwanzo wa urafiki mkubwa kati ya Happy na Michelle. ENDELEA............................ Urafiki kati ya Happy na Michelle uliendelea kuimarika siku hadi siku.Michelle alijitahidi kadiri alivyoweza kuwa karibu na Happy .Kila mwisho wa wiki walitoka na kwenda sehemu mbali mbali za starehe lengo likiwa ni kumchangamsha Happy.Pamoja na mambo hayo yote ambayo Michelle alijitahidi kufanya ili kumfanya Happy awe na furaha lakini haikuweza kumsahauliasha kuhusu Patrick hata nukta moja.Alijitahidi kila awezavyo ili asiweze kumsahahu kijana huyu mwenye upendo wa ajabu kwake. Ili tokea siku moja chuo kikafungwa kwa muda wa wiki mbili,Michelle akamuomba Happy wazitumie wiki mbili hizo kwa kuitembelea familia yao huko California.Happy akakubaliana na mwaliko huo na kesho yake wakapanda ndege na kuelekea California.Walipewa mapokezi mazuri na familia ya akina Michelle.Ilikuwa ni furaha iliyoje kwao kumpata mgeni aliyetoka Tanzania. . Siku mbili tu baada ya kuwasili kwao hapo nyumbani ,Mike naye akawasili akitokea jiji la New York anakofanya kazi.Tayari alikwisha taarifiwa na mdogo wake Michelle kuwa tayari Happy alikuwa hapo nyumbani kwao.Mike aliwasili mida ya mchana na kuwakuta familia nzima ikiwa imejipumzisha.Akasalimiana na wote kisha akaelekea chumbani kwake.Kijasho kilikuwa kikimtiririka hasa baada ya kulishuhudia kwa mara ya kwanza tabasamu pana la Happy .Alikaa kitandani na kujaribu kuwaza ni jinsi gani atakavyoweza kujiweka karibu na binti huyu mwenye urembo usioelezeka..Alishindwa kupata jibu akaamua kwenda kuoga kisha akaelekea bustanini ambako Michelle na Happy walikuwa wamepumzika kwa muda huo. Mara tu baada ya Mike kuwasili hapo bustanini ,Michelle akainuka na kwenda ndani kuongeza vinywaji,akawaacha Mike na Happy .Mike moyo ulikuwa ukimdunda .Ilihitaji ujasiri wa aina yake kuanzisha maongezi na binti huyu mwenye uzuri wa kimalaika.Baada ya kimya cha sekunde kadhaa toka amefika pale Mike akajikaza kiume na kuanzisha maongezi. “Happy unanikumbuka?” :Happy akanyamaza kidogo kana kwamba anajaribu kukumbuka kitu kisha akajibu. “hapana” “Nilikuja siku moja chuoni kwenu nikakukuta umeiinamia kompyuta yako” akasema Mike na Happy akatabasamu “Ouh ! nimekukumbuka.kumbe ni wewe ! Samahani siku ile sikuwa katika hali nzuri ndio maana sikukujibu vizuri.” Akasema Happy huku akitabasamu “.hata mimi nilijua haukuwa katika hali nzuri kwa sababu siku hazifanani.” Mike akasema huku akatabasamu baada ya kumuona Happy akitabasamu “Vipi unaionaje hali ya Marekani”Mike akauliza “ ni nzuri,Marekani kuzuri,kila kitu kizuri ,but I miss home” akajibu Happy “Tanzania? Mike akauliza ‘Yes ! nani kakwambia kuwa natokea Tanzania? ‘Michelle” Mike akajibu .Happy akatabasamu “Hata mimi” Mike akaendelea “naipenda sana Tanzania.Nasikia ni nchi ya amani na watu wake ni wakarimu mno.” Happy akatabasamu baada ya kauli ile ya Mike “Nafurahi kusikia hivyo.Umekwisha wahi tembelea nchi yoyote ya Afrika? Akauliza Happy “Hapana bado sijatembelea nchi yoyote ya Afrika. Ila nina mpango wa kufanya ziara Afrika na nchi ya kwanza kutembelea itakuwa Tanzania.” “Nini kinakuvutia mpaka uifanye Tanzania kuwa nchi ya kwanza kuitembelea? Happy akauliza “Just to see pretty women” Mike akajibu na wote wakaangua kicheko. “ Nina hakika Tanzania imebarikiwa kwa kuwa na vivutio vingi vya kiasili lakini hata hivyo kuna wasichana warembo mno” akasema Mike na wote wakaendela kucheka. Ilikuwa ni wiki nzuri sana kwa Happy .Alifurahi kukutana na familia yenye watu wakarimu kama hii ya akina Michelle.Kwa kiasi Fulani ziara hii ya California ilisaida kumuondolea msongo wa mawazo uliokuwa ukimkabili.Mike na Michelle walijitahidi kwa kila walivyoweza kuhakikisha kuwa Happy anakuwa na furaha kwa muda wote atakaokuwa hapo kwao. Jumapili Mike akamuomba Happy watoke kwa ajili ya matembezi.Michelle alikuwa hajisikii kutoka.Jioni ya siku hiyo wote wawili wakiwa wamependeza vilivyo walipanda gari na kutoka.Safari iliishia katika klabu moja kubwa na maarufu .Ilikuwa ni sehemu tulivu na yenye mandhari ya kuvutia mno.Waliagiza vinywaji na kuanza kunywa taratibu huku wakiendelea na maongezi ya hapa na pale.Kisha Mike akabadili maongezi na kusema. “Happy leo ni siku ya furaha sana kwangu kuwa karibu nawe katika mahali tulivu kama hapa na ni siku muhimu vile vile kwa kuwa nimedhamiria kuutua mzigo mzito unaonikabili kwa muda mrefu sasa” Happy akastuka kidogo kwa kauli ile ya Mike lakini akamuacha Mike aendelee. “Happy nina furaha moyoni mwangu kukutamkia kuwa u mwanamke pekee ambaye umeweza kuuteka moyo wangu kwa kiasi ambacho siwezi elezea.Kwa ufupi Happy nakupenda sana na tafadhali ninaomba uridhie ombi langu la mimi na wewe kuwa wapenzi.Naomba unielewe Happy kuwa penzi langu kwako ni la dhati lenye lengo la kuja kuishi nawe kama mume na mke pindi utakapomaliza masomo yako.” Happy akaiweka glasi chini ,akamuangalia Mike kana kwamba ni mara ya kwanza anamuona.Mike naye akamuangalia Happy kwa makini Happy akatabasamu ,tabasamu ambalo kwa kiasi kikubwa linamchanganya Mike. “Mike you are very handsome” Happy akasema akainua glasi yake ya kinywaji akanywa funda moja “Oh ! thank you Happy” mike akasema huku akitababasamu na kuirekebisha tai yake aliyokuwa amevaa.Happy akaendelea “ Mike wewe ni kijana ambaye kila mwanamke angependa uwe naye.Una kila sifa za kijana bora.U mcheshi,mchangamfu na unayevutia.Nashukuru kwa kuwa wazi na hisia zako.Ila samahani kaka yangu mimi tayari nina mtu ambaye sijui hata nikuelezeje ili unielewe kwa jinsi ninavyompenda Kijana huyu ndiye aliyeushika moyo wangu,ameyashika maisha yangu.yeye ni kila kitu kwangu.Nampenda Patrick kuliko ninavyojipenda mimi.Kama nisingekuwa na Patrick nisingekukataa Mike.” Happy akasema kwa kujiamini. Mike akainama chini kwa sekunde kadhaa akiwaza.tayari alikwisha uona ugumu uliopo mbele yake.katika kumshawishi Happy akubali ombi lake la kuwa naye katika mahusiano. “Happy naheshimu mawazo yako na ninauheshimu sana uhusiano wa mtu.Si lengo langu kuvuruga uhusiano wako.Kwa kuwa tayari una mpenzi anayekupenda na wewe unampenda basi naomba kitu kimoja tu kutoka kwako.” “Kitu gani Mike?” Happy akauliza “ nataka tuwe marafiki wa kawaida” “Kwa hilo hakuna shida.Mike nashukuru sana kwa kunielewa.Nitakuombea ili uweze kumpata msichana kama mimi ambaye nina imani utampenda zaidi yangu.” “nafurahi kusikia hivyo Happy ” Mike akasema katika hali ya unyonge. Maisha yaliendelea vizuri na baada ya wiki mbili kumalizika Michelle na Happy wakarudi chuoni Mike akarejea kazini kwake New york **************************** Patrick aliendelea na maisha ya gerezani kama kawaida.Siku moja Patrick akaitwa na mkuu wa gereza na kuambiwa ajiandae kwa safari alikuwa akihamishwa gereza.Hii ilikuwa ni taarifa ambayo ilimvunja moyo sana kiasi cha kumfanya adondoshe machozi.Ni wafungwa watatu tu ndio waliokuwa wakihamishwa gereza. Haikuweza kufahamika mara moja sababu ya kuhamishwa kwao Wakati wakijiandaa kuondoka ,hakukuwa na mfungwa mwingine wa karibu ambaye angeweza kumwachia ujumbe wowote.Hakujua anahamishiwa gereza gani. Alizoea kila wiki kupokea barua za Happy .Hakujua angewezaje kumfahamisha juu ya uhamisho ule wa ghafla. Safari ilianza bila kuchelewa .Ilikuwa ni safari ndefu na yenye kuchosha.Gari walilopanda lilikuwa na madirisha madogo juu kwa ajili ya kuingiza hewa .hivyo kutokutambua ni wapi walikokuwa wakielekea. Wakiwa wamepitiwa na usingizi walistuliwa na sauti ya kufunguliwa kwa mlango.Walifunguliwa pingu walizokuwa wamefungwa mikononi na kuamriwa kushuka.Walikuwa wamechoka kupita kiasi.Ilikuwa ni safari ndefu na njaa ilikuwa ikiwauma kupita maelezo.Tangu wapewe chakula mchana ambacho kilikuwa ni chipsi kavu na maji ya kunywa hawakula tena chochote. Tayari giza lilikwisha tanda angani.Hawakujua ilikuwa ni saa ngapi mida hiyo.Hali ya mahala hapo ilikuwa ni ya baridi kali.Wote walikuwa wakitetemeka.Walisimamishwa hapo kwa takribani dakika ishirini kisha askari mmoja akatoka ndani akawaangalia na kuamuru wapelekwe ndani wakapumzike.Waliongozwa na askari wawili wenye silaha hadi ndani ya gereza.Kila mmoja akaonyeshwa chumba chake cha kulala.Hili lilikuwa ni gereza jipya kabisa na la kisasa lililokuwa limejengwa mjini songea kwa msaada wa watu wa Marekani.Lilikuwa ni gereza la kwanza la mfano nchini Tanzania kuwa na ubora wa hali ya juu afrika mashariki na kati.Patrick alishukuru Mungu kwa kuletwa hapa .Kutokana na uchovu wa safari aliokuwa nao akajitupa kitandani na kulala. Saa kumi na mbili asubuhi king’ora kikalia .Patrick mwili wote ulikuwa ukimuuma kwa uchovu na alihisi njaa kali. “Hey amka ndugu ” Akastuliwa na sauti ya mtu aliyekuwa akimtikisa.Akafumbua macho na kukutana na macho ya kijana mdogo mwenye sura ya upole. “Vipi husikii king’ora hicho?” Akaendelea kusema yule kijana. Kiuvivu Patrick akainuka na kukaa kitandani.baada ya kama dakika tatu hivi akaja askari akafungua geti la chumba chao na kumrushia Patrick nguo mpya kabisa za kifungwa.Hakusema kitu akazikunjua na kuvaa . “Kwa hiyo nini kinaendelea saa hizi? Utaratibu wa hapa ukoje ?” Patrick akamuuliza yule kijana waliyekuwa wakilala wote chumba kimoja. “huu ni muda wa kujiandaa,kunawa au kuoga kama unataka .Kitapigwa king’ora kingine tutaenda kupata mlo wa asubuhi halafu baada ya hapo tutapangiwa kazi.” Patrick akaonyeshwa sehemu yenye mabafu akaingia na kuoga..King’ora kingine kikalia na wote wakakusanyika katika bwalo la chakula kwa ajili ya kifungua kinywa..Walikuwa wafungwa wachache kama arobaini hivi. Baadaye kazi zikapangwa na Patrick na wenzake wakapangiwa sehemu ya kufyeka.Miongoni mwao alikuwemo yule kijana anayelala naye chumba kimoja.Walifanya usafi huku wakisimuliana mambo mengi na kupeana moyo.taratibu wakaanza kuzoeana na kujenga urafiki. Usiku wa siku hiyo Patrick na yule kijana ambaye alikuja kumfahamu kama Andrew waliutumia katika kusimuliana mikasa mbali mbali ya maisha yao.Andrew alimsimulia Patrick kisa cha yeye kuwapo pale gerezani.Kifungo chake kilikuwa cha miaka mitatu na kilitokana na kusababisha ajali wakati akiendesha gari akiwa amelewa. Patrick naye alimsimulia hadithi yake na mpaka anamaliza Andrew alishindwa kujizuia kudondokwa na mchozi. “Pole sana Patrick hayo yote ni majaribu katika maisha .Ni wazi Patrick una upendo wa dhati na wapekee sana kwa huyo Happy .Usikate tamaa Mungu atakusaidia utamaliza kifungo chako.” “Ahsante sana Andrew kwa kulitambua hilo na kunipa moyo.Lakini kitu ambacho bado kinaniumiza sana kichwa ni jinsi nitakavyoweza tena kuwasiliana na Happy .Katika gereza lile nilikotoka ,mkuu wa gereza alikuwa amejitolea kunisaidia kwa kutuma barua zangu kwenda kwa Happy na kupokea zitokazo kwa happy na kuniletea..Ningeweza kuwatumia wazazi wangu lakini bado hawajui kama nimehamishwa gereza “ akasema Patrick kwa masikitiko ITAENDELEA SEHEMU IJAYO
Posted on: Tue, 19 Nov 2013 14:00:00 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015