Riwaya: NIACHE NA MOYO WANGU Sehemu: 07 Mtunzi: Andrew - TopicsExpress



          

Riwaya: NIACHE NA MOYO WANGU Sehemu: 07 Mtunzi: Andrew Carlos Simu: 0713 133 633 Ilipoishia… Gongo la kutembelea vizuri kwakuwa alikuwa na mguu mmoja. Alimbeba yule mtoto bengani akiwa ndani ya lile begi nakuanza safari yake uku mkono mmoja akiwa ameshikilia kidumu cha maji nakutokomea zake kusikojulikana. Songa nayo sasa… Levina hakulijali baridi la msitu wa Kakamega kwani ndani ya masaa machache aliyokuwepo alikuwa tayari ameshalizoea. Msitu wa Kakamega ulikuwa ukitisha kwa milio ya ajabu ya wanyama na ndege wa porini lakini kwa Levina masikio na moyo wake ulishajijenga kikakamavu. Ushupavu! Hakuogopa kitu maishani mwake.Aliona bora afe kishujaa. Alikuwa ameshajitolea kwa lolote litakalomkuta mbele yake yamkini alikuwa na mguu mmoja. Mguu mmoja uliokuwa ukisaidiwa kujikongoja kwa kutumia gongo na mgongoni akiwa amembebelea mtoto mdogo kwenye kabegi alikoachiwa na Osusu. Baada ya kuweza kujisogeza kamwendo kidogo Levina akajihisi kuchoka sana. Akakaa mpaka chini kwa uchovu uku yule mtoto akimshusha mpaka chini kutokea begani. Akamchungulia, alikuwa tayari ameshapitiwa na usingizi mkali. Levina alionesha tabasamu uku vidole vyake akivitumia kumpapasa yule mtoto usoni mwake. “Mtoto mzuri” Alijisemea Levina kwa sauti ya chini chini. Hakutaka kupoteza muda hata kidogo kwani aliamini kabisa kuchelewa kupumzika kwake kunaweza kuwafanya kina Butiliasi wakamkuta hapo msituni. Na hivi walikuwa hawatabiriki aliona wanaweza hata wakamduru tena. Baada ya kupumzika kidogo alimchukua tena yule mtoto kama alivyofanya awali nakumdumbukiza kwenye kile kibegi kisha akamuweka begani na kuendelea na safari yake kwa kutumia msaada wa gongo upande mmoja. ******* “Nawauliza tena bado mnataka kunifahamu?” Si Butiliasi, Papii, Osusu wala wale mateka wote walikuwa hoi. Walikuwa wamepelekwa gwaride la kutosha na mzee mwenye kijiji. Mzee mwenye msitu, Mzee wa siku nyingi katika msitu wa Kakamega, Aguati mwana wa thorong’ong’o. “Kama kweli wewe ipo mwanaume, ebu batokelezee tukueneshe? Kata utum mmbo,tupilia m mmbali!” Alisema Butiliasi kwa hasira na kigugumizi cha muda. Aguati alichowafanyia safari hii alitokea hadharani. Wote wakamshangaa kwa jinsi alivyo na ngozi nyeupe sana. Nywele ndefu kutokea masikioni. Na nyusi zilizokuwa zimejawa na mvi nyeupe na nyeusi. “Mmeniona?” Alinenea Aguati. “Ndio” Butiliasi alijibu kwa kujiamini. Alikuwa kama mwanaume aliyelishwa pilpili kali mdomoni mwake. Alishajitolea kwa lolote liwe ili mradi aweze kumuua kiongozi wao mkuu. Kiongozi wanayemtegemea na kumtukuza wana Kakamega. Alichowafanyia Aguati. Alinyoosha mikono yake miwili nakuielekeza eneo walipokuwa kina Butiliasi na wenzake. Kisha ile mikono akafanya ishara kama anataka kunawa. Wale kina Butiliasi wote wakabaki kama wakikumbatiana. Wakakunjamana! Wakagusana kila mmoja kwa kushikana mikono. Wote wakawa kitu kimoja. Baada ya hapo Aguati akawaburuza kwa kutumia ishara ya mikono. Wote wakajikuta wakitambaa kutokea nje. Hawakuweza kujinasua hata mara moja. Aguati akawa mstari wa nyuma uku wale kina Butiliasi wakiwa mbele yake akiwasukuma kimiujiza kutoka nje kwa kutumia ile ile ishara ya mikono yake. Kwa mara ya kwanza Butiliasi aliweza kutoa mchozi wa kuumia uku Papii na Osusu nao wakiyapokea maumivu kwa kutoa machozi ya kimya kimya. Mzee Aguati aliendelea kuwaburuta kuelekea msituni uku wakiwapitia baadhi ya wanakijiji wenzake ambao walikuwa wameshauliwa na Butiliasi kwa risasi kali. Butiliasi alishajua wazi wanapopelekwa lakini hakuwa na nguvu ya kufanya vyovyote zaidi ya kutoa tu sauti. “Aguati? Aguati?” Aliita Butiliasi kwa sauti ya juu . Aguati akashusha mikono yake miwili. Kina Butiliasi wakampumzika uku wakihema hoi kwa kupelekewa mchakamchaka. Wale mateka ni kama walikuwa na kizunguzungu cha muda kwani kitendo cha Aguati kushusha mikono walijikuta wote wakidondoka mpaka chini nakuanza kugalagala mithili ya mtu anayeugua ugonjwa wa kifafa. “Mnasemaje?” Aguati alihoji. “Unatupeleka wapi wewe muzee?” Aliongea Butiliasi kwa kujiamini. “Nawapelekeani kwa mungu, baba yangu. Baba amekasirika sana. Hawapendi! Tangu mmekuja uku nakuua ovyo amechukia sana sasa ni bora akawahukumu yeye mwenyewe.” “mungu gani?” Aliendelea kuhoji Butiliasi uku akili yake yote akijua wazi wanapopelekwa. “Shimoni, kwenye jiwe la kafara. Wacha baba yangu akawahukumu” Alimaliza kuongea Aguati kisha akafanya kama alivyokuwa akiwafanya awali. Aliinyanyua mikono yake miwili nakuweza kuwainua kwa kutumia ishara ya mikono kisha safari ya kuwapeleka ikaendelea. Butiliasi alipajua sahawia kwenye shimo la kutolea kafara. Lile shimo ambalo alimsukuma kiongozi mmoja wapo waliyekuwa wakimuita Otieno. Alikumbuka pia walivyotupwa waasi wenzake pamoja na mateka wote aliokuwa nao akiwalinda kwa muda mrefu sana toka Congo,Burundi,Rwana na Uganda. “Imeshakuwa muvita hii wacha tufe kwa muvita!” Alinena Butiliasi kimoyo moyo. Safari ya kupelekwa kwenye jiwe la kutolea kafara haikuwa ndefu sana. Baada ya dakika kadha walikuwa tayari tena juu ya lile jiwe uku Aguati akiwa pembeni yao. Wote walikuwa wakitetemeka mithili ya kifaranga cha kuku kikinyeshewa mvua ama kumwagiwa na maji. Si Papii wala Osusu wote suruali zao zilikuwa zimejawa na haja ndogo. Aguati alianza kwa kuwachukuwa wale mateka wote. “mungu yangu, wachukue hao ni zawadi kutoka kwangu!!” Aliongea Aguati uku akiwadumbukiza wale mateka wote waliokuwa bado na kamba mikononi mwao.Aguati akawadumbukiza. Shimo likawameza! Wakabaki watatu,Osusu,Papii na Butiliasi. “Tubadilishie adhabu tafadhali” Papii aliropoka. Butiliasi alikasirishwa na kauli ya mwenzake,Papii kujishusha mbele ya Aguati na mungu wao. Alichiokifanya,kwa hasira alimsukuma Papii kwenye shimo la kutolea kafara. Aguati akatoa meno kwa kucheka na mungu wao akajibu kwa kutoa sauti kali kutoka ndani ya lile shimo. Papii akawa amemezwa rasmi na mungu wa Kakamega. Wakabaki wawili Osusu na Butiliasi. “Aingiie mmoja hapo shimoni mungu anamtaka?” Aliongea Aguati uku akiwa amekalia jiwe pembeni ya shimo la kutolea kafara. Butiliasi akaanza kusukumiana na Osusu kuingia mule ndani ya lile shimo. Wote walikuwa waoga. Waasi wakusalitiana wenyewe kwa wenyewe. Walijiona ni bora wakakamatwa na wanajeshi wa nchi ama umoja wa mataifa kuliko kuwa hatiani na Aguati katika shimo lao la kutolea kafara. Walivutana muda mrefu bila hata ya mmoja kulisogelea lile shimo. Aguati akapata hasira sana kwa kutokwenda hata mmoja ikabidi awasogelee mpaka karibu. Kitendo cha kuwafikia karibu kina Osusu na Butilialsi pale pale wakatumia mwanya wakumgusa rasmi Aguati na kumsukuma. Aguati akajikwaa na kudondoka mpaka kwenye shimo la kutolea kafara. Kilichofuata hapo ni makelele yasio ya kawaida. Kijiji chote cha Kakamega kikalipukwa na kelele za ajabu. Mwanga mkali ukatoka mbele yao. Kisha kilichofuata ni kitu mithili ya radi kikaruka juu kabisa kutokea katika lile shimo na kupaa juu kabisa na kiliposhuka kilishuka karibu yao nakujitandaza. Kilikuwa ni kitu cha ajabu sana kisicho na mbele wala nyuma. Kilikuwa mnyama si mnyama na hata binadamu si binadamu. Osusu na Butiliasi wakaanza kurudi kinyume nyume wakiiogopa kile kiumbe cha ajabu. Kilikuwa na nguvu ya ajabu sana. Kikainuka na kuanza kuchomoza mikono yake mingi sana. Kikawa pweza si pweza wala ng’e si ng’e. “Mvrrooooo, Mvroooo!!” Hakikuweza kutoa sauti ya kueleweka zaidi ya mlio wa ajabu tena mlio kama wa pikipiki. Kikazunguka kwa nguvu zote nakusababisha eneo lote kuzungukwa na upepo mkali. Upepo usio wa kawaida. Osusu na Butiliasi wakawahi kuyashika mawe madogo kwa ajili ya kujizuia. Upepo ule ukawazidi nguvu. Wakapepea mpaka kukutana na miti chini kabisa. Wakakumbatia miti ndipo na ule upepo ukapungua nguvu. Wakaendelea kutolea macho kile kitu cha ajabu kilichokuwa kikiwapa adhabu.Kiliwaogopesha sana. Kilijizungusha tena hewani na safari hii kilipotua kilikuwa kikubwa zaidi na kuwa na vichwa vya watu wengi sana mwilini. Sura za watu mbali mbali ziliweza kuonekana sambamba na macho yao na midomo wakiikenua kwa kucheka. Butiliasi aliweza kuona sura za waasi wenzake. Machozi ya huruma yalimwingia. Moyo wake Ukalalama! lakini hakuwa na jinsi katika himaya ya watu. Alikuwa ni mtu wa kusubiri miujiza itokee. Baada ya kile kiumbe kujizungusha taratibu kwa muda. Kiliongoza mpaka kwenye shimo la kutolea kafara. Kukabaki kimya kabisa. Butiliasi aligeuza macho yake kumwangalia mwenzake Osusu lakini hakuweza kumuona. Akatetema kwa hofu! Woga ukamtawala upya. Macho akayatoa. “Osusu, Osusu naacha mimi?” Aliita Butiliasi kwa sauti ya juu na ya masikitiko. “Nipo mubosi yangu, nipo njoo?” Aliongea Osusu ambapo kwa uoga wake alikuwa amepanda juu ya mti kabisa na kujificha akiogopa. Butiliasi naye akataka kupanda juu ya mti ule lakini hakuweza kwakuwa mti ulikuwa ukiteleza sana. Hivyo akabaki akitolea macho eneo la shimo. Mvuke wa ajabu ukaaanza kutokea kwenye lile shimo. Ule mvuke ukapaa juu zaidi na uliposhuka ulitawala eneo lote la Kakamega. Miti yote ikaanza kupukutika majani yake. Mwanga wa ajabu ulioweza kugeuza usiku kuwa mchana. Hapakuwa na giza tena eneo lote lile. Kulikuwa kama kumeshapambazuka. Ukimya ulizidi kuwatetemesha Butiliasi na mwenzake Osusu. Muda wote hadi majani yakipukutika Osusu alikuwa akining’inia juu ya mti. Hakutaka hata kuteleza ama kuachia mti ashuke chini. Aliona kwamba mti ndio mtetezi wake aliyebaki. Baada ya kimya cha muda lile shimo likaanza tena kutoa maji si maji, uji si uji na hata damu si damu. Zikaanza kutiririka kwa kutawanyika eneo lote la Kakamega. Butiliasi kamwe asingeweza kuzikwepa zile damu damu. Zilikuwa kali sana hata zaidi ya tindikali. Ziliipitia miguu ya Butiliasi. Ikameguka yote. Butiliasi akadondoka mpaka chini napo zile damu zikammeza zote. Akamalizwa mwili wote mpaka na nguo zake zikateketea pale chini. Butiliasi akawa ameshaaga dunia rasmi. Utawala wa dakika chache ukabaki mikononi mwa Osusu. Osusu ambaye alikuwa bado amening’inia juu ya mti. Alikuwa akishuhudia tukio lote la kumalizwa kwa kiongozi wake wa muda mrefu wa kikundi chao kilichosumbua sana nchini Congo. Kikundi cha waasi kiilichoyashinda majeshi ya Uganda, Kenya , Rwanda,Burundi na hata nchini kwao Congo. Kikundi kikubwa cha M23. Osusu hakuwa na furaha hata kidogo. Aliendelea kutoa macho nakuangalia zile damu zikimalizia theluthi ya shati la Butiliasi. Baada ya kumaliza kila kitu,zile damu zikahama tena. Zikaanza safari ya kuelekea juu ya mti alipokuwepo Osusu. “Mie siyo mutu ya Congo bana! mie sio muasi! mie sipo na Buti.. mim ni mateka.. mie sio mutu ya bolingo nangai !!” Osusu alijikuta akiongea lugha isiyoleweka. Alijikuta akiziambia zile damu zisimfuate. Alijikuta hata akisaliti cheo na alipotoka. Zile damu zilizidisha nguvu na kasi ya kupanda juu. Zilimfikia Osusu na kumteketeza kwa kumuingia mwilini. Osusu alibaki mifupa mitupu. Nayo ile damu haikukubalina na mifupa. Ikaiteketeza mifupa yote. Osusu akawa ameshafariki rasmi. Hivyo utawala wa muda wa waasi katika Msitu wa Kakamega ukamalizwa na kitu cha ajabu kutoka katika shimo lao la kutolea kafara. Ile damu ilipomaliza kumtetekeza Osusu haikutosheka. Ikaingia msituni kwa ajili ya kutafuta chochote itakachokutana nacho. Ikaanza safari ya kwenda kwa kasi uku ikiteketeza miti yote nakuwa patupu. Ilizidi kusonga na kukata mbuga. ***** Upepo ulizidi kuwa mkali zaidi. Anga nalo lilionekana kama kuchafukwa eneo lote. Ile mbalamwezi hafifu iliokuwa ikiangaza nayo ilifutika ghafla na kubaki na mwanga mkali sana. Levina alisimama na kugeuka nyuma. Alikaa chini na kumshusha mtoto kisha akafungua ile zipu aliyokuwa ameifunga kidogo kuachia eneo dogo la mtoto kupata hewa. Levina alimchungulia yule mtoto. Alikuwa bado amepitiwa na usingizi mzito sana kwa kushiba. Levina akaliruidishia begi lake. Mwanga mkali ukaendela kuliteka eneo lake. Akajikuta ghafla kumepambazuka na kuwa mwanga kama vile machana na sio asubuhi. “Ohhh asante Mungu, ama kweli wewe waweza!” Levina alishukuru kimoyo ,moyo uku akiliweka lile begi mgongoni. Begi lililokuwa na mtoto kisha akachukua gongo lake na kuendelea na safari. Safari ambayo kwa sasa ilimsaidia kutokana na kupambazuka kwa eneo. Pili aliweza kuona njia ya wapitao kwa miguu. Alizidisha mwendo uku akiamini wazi atakutana na barabara ya lami. Barabara ile ya kipindi kile walioiacha nakushinikizwa na waasi wapitie msituni wasiifuate barabara ya lami. Baada ya mwendo kidogo levina alichoka sana kutokana na maumivu mfululizo ndani ya mwili wake. Mabega yalikuwa hayafanyi kazi kutokana na kumbeba mtoto pia mabega hayo hayo yalikuwa yamefungwa na kina Kakamega walipompa adhabu kipindi kile kwenye himaya yao. Paja lake moja lile ambalo mguu ulikuwa haupo ulianza kumletea tabu sana. Ikambidi levina ajikokote kwa kujiburuta chini taratibu uku akiliacha gongo lake. Mkono mmoja aliutumia kwa kuburuta begi na mwigine aliutumia kwa kujivuta yeye mwenyewe taratibu. Kwa mbali badaa ya kujiburuta si mwendo sana macho yake kwa upande wa mbele yaliweza kuona gari dogo likikatisha. Levina akalinyooshea mkono lakini lile gari lilikuwa na mwendo kasi halikuwaeza hata kuona kitu. Nguvu zikamrejea Levina japo hazikuwa nguvu sana akaanza kujiburuta haraka haraka kitendo cha kuifikia barabara ya lami tu uku akiwa na kile kibegi alishangaa kwa nyuma yake kusikia sauti ya ajabu. Sauti ya kama upepo uvumao kwa kasi. Aliyageuza macho yake lakini alichoweza kuambulia ni kuona tambalare. Msitu wote ulikuwa umeshamezwa. Umemezwa na damu damu nyekundu si nyekundu na hata nyeupe si nyeupe. Zile damu zilikuwa zikitoa mvuke wa ajabu kama maji yachemkao kwa kasi. Ule mvuke ukafanya ile damu kupoa na ghafla ikapunguza kasi. Zie damu zikamsogelea Levina zikiwa zimepoa kabisa,hazikuweza kudhuru kama zilimvyowafanya Butiliasi na Osusu. Kilichofanyika zile damu zilimtanda mwili mzima Levina uku zikiliacha lile begi lililokuwa na mtoto mdogo. Hazikuweza kumdhuru mtoto wala Levina. Zilimzunguka kwa muda kidogo kisha zile damu zikanywea na kuondoka zake zikirudi msituni. Kwa jinsi zilivyokuwa zikirejea ndipo na msitu ule ukaanza kujijenga upya na kuwa msitu zaidi. Majani yakarejea upya haraka haraka msitu ukarudi kama ulivyokuwa awali. Baada ya muda kidogo kelele za watu zikasikika kama wakishangilia ushindi. Makelele yale yaliufunika msitu wote. Levina akawakumbuka sana wana Kakamega. Akaamini huenda zile damu baada ya kuja kwake zimeenda kupeleka amani. Levina akawa kama mtu asiyejiamini. Alitetemeka sana mwili mzima. Akajikuta akilala chini na kupoteza fahamu uku naye yule mtoto aliyekuwa kwenye begi akitoa makelele ya kulia kutoka usingizini. ****** ::: Mwisho wa utangulizi wa Riwaya hii kali na ya kusisimua. Kamwe usithubutu kuikosa hii hata siku moja kwani ni zaidi ya tamthiliya, zaidi ya movie za kivita na hata za kutisha,mapenzi na kipelelezi. Ni Riwaya yenye kukuhuzunisha, kukuliza, kukupa midadi na hata kukuogopesha na kukufuruhisha. ::: Kesho ndio tutaanza rasmi na Riwaya hii ya NIACHE NA MOYO WANGU sehemu ya kwanza na itakuwa ikitoka kila siku kasoro siku ya jumapili. ::: Gonga LIKE na pia usisahau ku COMMENT kama imekugusa riwaya hii ya NIACHE NA MOYO WANGU. ::: SHARE nyingi zaidi zitakufanya ewe msomaji niwe nakutagia hii Riwaya kila itokapo. Unachotakiwa kufanya ni Ku SHARE mara nyingi uwezavyo na yeyote atakaye SHARE zaidi ya mara 2 nitakuwa nikimtag kila inapotoka. ::: Tukutane tena kesho mida kama hii.
Posted on: Mon, 11 Nov 2013 07:26:27 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015