SIMULIZI; CHURA NAMBA 20! MTUNZI; IBRAHIM GAMA. SEHEMU YA - TopicsExpress



          

SIMULIZI; CHURA NAMBA 20! MTUNZI; IBRAHIM GAMA. SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU. 0718603654/ 0764596554. 455. Sababu sikuwa hivi, Siutumii ulevi, Sina uzee wa mvi, Vipi nguvu zanishia?! 456. Ninasafiri ‘bondeni’, Nakujaza mdomoni, Mikono ikifuwani, Matiti inachezeya! 457. Huku ndo mzuka wake, Sababu kelele zake, Ukitaka usitake, Mnazi utaukwea! 458. Kwa dakika thelasini, Kukawa kudogo ndani, Eneo gani mwilini, Lililokosa fikiwa?! 459. Nina miaka miwili, Sijaifanya shughuli, Leo kiwanja cha mbali, ‘Mjinga’ nashangilia! 460. Namtazama usoni, Amewiva kama nini, Hafumbuwi zake mboni, Raha zimemkolea! 461. Mie moto nimepamba, Jogoo ayumbayumba, Kuchi popote hutamba, Kupoa anakawia! 462. Tatizo hivi alivyo, Naharibikiwa hovyo, Anapambana vilivyo, Nimuwekavyo akaa! 463. Kwake sijaisikia, “Nimechoka” kunambia, Mtundu hajatulia, Huyu Kungwi nawambia! 464. Yani mama Khalfani, Nilinganishe na nani, Kwani hata Jasmini, Mbali atasubiria! 465. Leo hakuna kulala, Ni pambano la Kabwela, Dhidi yake Kabaila, Majogoo yaamua! 466. Hadi kunapambazuka, Nyang’anyang’a tumechoka, Hakuna anekumbuka, Goli alojifungia! 467. Mechi imemalizika, Ndipo ninapokumbuka, Kinga hazikutumika, Vipi kama kaumia?! 468. Waniruka usingizi, Mwili unakufa ganzi, Alishatuweka wazi, Viwanja kahudhuria!!! 469. Sasa ninajilaumu, Mjinga nilohitimu, Nae hakunilazimu, ‘Condoms’ kuzitumia! 470. Mtu asienijuwa, Awezaje kuamuwa, Pasi kinga kuvaliwa, Au yeye kauvaa?! 471. Sina hakika uzima, Au wake usalama, Kwa macho siwezi pima, Vipimo vitaamua! ******* 472.”Hodi hodi humu ndani, Kwanza nawasalimuni, Zatoka jana jamani, Uchovu umeshapoa?” 473. Mwenyeji anaingia, Huku atusalimia, Nasi twamuitikia, “Karibu” tunamwambia. 474. Mikono tunapeana, Hujambo twaulizana, Twazungumza kwa kina, Hatua za kuchukuwa! 475. Saa saba adhuhuri, Tumeshashiba vizuri, Twaingia kwenye gari, Kwa mwenyeji twaendea. 476. Watu wanne garini, Twaondoka Kaloleni, Twaelekea kusini, Mwenyeji anapokaa. 477. Stendi tunapapita, Kona kadhaa twakata, Mwisho wake tunagota, Njiro tunaposhukia. 478. “Tafadhali karibuni, Naomba piteni ndani, Kuweni huru wageni, Chochote kukitumia!” 479. Nyumba kubwa ya fahari, Ipo mahala pazuri, Utajapo nyumba nzuri, Na hii inaingia! 480. Sebuleni tunakaa, Vitu vimetapakaa, Fenicha zimezagaa, Zote ni za bei mbaya! ITAENDELE TENA KESHO.
Posted on: Fri, 23 Aug 2013 04:43:45 +0000

Trending Topics




© 2015