SOMETIMES I HATE THIS OUR COUNTRY KENYA BECAUSE WE INVOLVE - TopicsExpress



          

SOMETIMES I HATE THIS OUR COUNTRY KENYA BECAUSE WE INVOLVE POLITICS EVEN IN EDUCATION ISSUES WHY? WHY THEY FAIL TO RUNK MARANDA POLITICS EISH POLITICS WILL NEVER TAKE US ANYWAY EVERYTHING HAS ITS OWN TIME NIMESEMA NIMESEMA SHULE 36 za kitaifa na za ngazi ya kaunti hazikuorodheshwa kwenye matokeo ya mtihani wa KCSE ya mwaka jana baada ya wanafunzi wengi kujihusisha katika udanganyifu. Aidha, shule hizo zilikosa kuripoti visa hivyo kwa Baraza la Kitaifa la Mitihani (KNEC). Shule hizo ziko katika kaunti za Siaya, Meru, Nairobi, Tana River, Wajir, Homa Bay, Kisii, Nyandarua, Migori, Kisumu, Busia, Narok, Nandi na Mandera. Afisa Mkuu Mtendaji wa KNEC Paul Wasanga aliambia wanahabari kwamba shule ambazo wanafunzi walihusika katika udanganyifu hazikuorodheswa ila tu katika visa ambapo waliodanganya walikuwa chini ya watano. “Hakuna shule yoyote ambayo ililengwa. Shule ya Maranda haikuorodheshwa kwa sababu wanafunzi 23 walihusika katika udanganyifu somo la kompyuta,” alisema. Alieleza kuwa katika mtihani wa KCSE wa mwaka 2012, shule ya Maranda iliorodheshwa licha ya kwamba ilikuwa na mwanafunzi mmoja aliyedanganya. Bw Wasanga alieleza kwamba katika shule ambazo walimu wakuu waliripoti visa vya wizi kwa baraza, na wanafunzi walioiba wakawa chini ya 10, shule hizo ziliorodheshwa. Mfano wa shule hizo ni Pangani Girls ya kaunti ya Nairobi ambapo watahiniwa 7 walihusika katika udanganyifu. Mwalimu mkuu wa shule hiyo hata hivyo aliripoti kwa KNEC na shule hiyo iliorodheshwa. Bw Wasanga alimsifu sana mwalimu mkuu wa shule hiyo Pacifica Nyambongi kwa kujitolewa kukabiliana na wizi wa mitihani. Alisema hii si mara ya kwanza kwa shule kukosa kuorodheshwa kwa sababu ya wizi wa mitihani na kwamba hakuna siasa zilizotumika kukosa kuorodhesha baadhi ya shule, kwa mfano Maranda. Wabunge kutoka eneo la Nyanza wamekasirishwa na hatua ya kutootodheshwa kwa Maranda, na walilalamika bungeni na suala hilo likakabidhiwa kamati ya elimu bungeni. Waziri wa Elimu Jacob Kaimenyi ametakiwa kufika mbele ya kamati hiyo Machi 19 kufafanua hilo. Shule ya Maranda ndiyo iliyoongoza kitaifa katika mtihani wa KCSE wa 2011.
Posted on: Sat, 15 Mar 2014 08:01:25 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015