SOMO :Maeneo Unabii Unapotokea Huko Ulimwengu wa roho. Wakati - TopicsExpress



          

SOMO :Maeneo Unabii Unapotokea Huko Ulimwengu wa roho. Wakati huu ningependa nikufundishe maeneo unabii unapotokea ulimwengu wa roho ili ikusaidie kufahamu ili na wewe uweze kuwa msaada katika huduma yako au mahali unaposali kwa faida ya mwili wa Yesu Kristo. Aina za Unabii ni kama ifuatavyo:- 1. Unabii unaotokana na Mungu aliye Hai. 2Nyakati 18:12,13 “Mikaya akasema , kama aishivyo BWANA,neno lile atakalolinena Mungu wangu, ndilo nitakalolinena’ Unabii wa aina hii unatoka moja kwa moja kutoka mbinguni kwa Mungu aliye hai, na kuwafikia watu wake hapa duniani. 2. Unabii unaotokana na mawazo yako. Mwanadamu katika mawazo yake, ndani ya fikra za kibinadamu anaweza kutabiri au kusema kuwa ametumwa na Mungu, lakini ikawa siyo kweli bali ni mawazo yake binafsi, yamemtumikisha na kutoa unabii uliotokana na mawazo yake. Yeremia 23:15-18 “Bwana wa majeshi asema hivi, msisikilize maneno ya manabii wakiwatabiria, huwafundisha ubatili,; hunena maono ya mioyo yao wenyewe, hayakutoka katika kinywa cha BWANA”. 3. Unabii unaotoka kwa shetani. Neno la ajabu katika mambo ya kiroho ni hili; shetani na yeye, anaishambulia sana ofisi ya unabii kwa kuingiza maneno yake katika mtiririko wa unabii unapoteremka hapa duniani. Ndio maana inalazimu kila unabii upimwe kabla ya kufanyiwa kazi kanisani au kwenye maombi ili kuzuia mkono na mtirirko wa shetani au wa kipepo usijipenyeze na kuleta udanganyifu au uharibifu Fulani. Ukisoma 1korintho12:10 unataja karama kadhaa, ikiwemo karama ya kupambanua roho. Karama hii inafanya kazi ya kuzitambua, roho takatifu au chafu zilizojipenyeza wakati wa ibada, maombi, au ziko ndani ya mtu Fulani aliye kati yenu. Lakini maneno haya yanaitaji mwalimu mwenye uzoefu katika mambo ya karama na huduma, na aliye jaa Roho Mtakatifu, ili asaidie kunyoosha kila neno kwa ufunua na kuyaweka mashauri vizuri. Ezekiel 13;9 “ Na mkono wangu utakuwa, juu ya manabii wanaoona ubatili na kutabiri uongo, hawatakuwa katika mashauri ya watu wangu” wala hayataandikwa katika maandiko ya nyumba ya Israel, wala hayataingia katika nchi ya Israeli nanyi mtajua yakuwa mimi ndimi Bwana MUNGU Tahadhari Kwa manabii: Ili kuweza kuepuka, maneno ambayo yanaweza kuleta uharibifu, na udanganyifu utakao leta uharibifu kanisani, zingatia haya yafuatayo yatakusaidia sana: i. Epuka tama ya fedha itakayo kushawishi vibaya na kuleta uharibifu. ii. Epuka mali za aibu, kutoka kwa wale uliowaombea na kuwatabiria. iii. Epuka kusifiwa ovyo ovyo, hasa na wale waliopokea uponyaji baada ya kuwatabiria na kuwaombea. iv. Kumbuka kurudisha utukufu na heshima kwa Yesu Kristo baada ya kila muujiza utakaotendeka katika utumishi wako. v. E puka fedha za udhalimu ambazo zitakuvunjia heshima wewe na jina la Yesu. vi. Kila mtumishi mwenye kipawa cha unabii akumbuke ya kuwa; Kitu kilichomfanya shetani aanguke ni kupenda sifa na cheo. Haya yameangusha Manabii wengi wazuri wengi na hawatainuka tena. Na Shetani aliangushwa kwa kutaka awe kama Mungu. Kila anayetumikishwa na Mungu Aliye hai katika Huduma ya Unabii, inbidi azingatie sana maelezo haya katika waraka huu, kwa ajili ya ustawi na mashangilio ya Kipawa cha Unabii kilicho ndani yake. Isaya 14:12-14 Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi, jinsi ulivyokatwa kabisa! Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, nitakiinua kiti changu kuliko nyota za Mungu; nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, katika pande za mwisho za kaskazini, Nitapaa kupita vimo vya mawingu Nitafafanana na yeye aliye juu. vii. Nabii ni lazima aepuke kusifiwa kila mara,kujivuna, na kujikweza na maisha ya anasa inayotokana na kuombaomba fedha za aibu. Kumb 7:25 “Pesa sanamu za kuchonga za miungu yao mtaziteketeza kwa moto; usitamani fedha wala dhahabu iliyo juu yao, wala usiitwae iwe yako, usije ukanaswa nayo; kwa maana ni machukizo kwa Bwana Mungu wako”. Yako mambo yanayopasa tuyaepuke kwani yataweza kutupunguza nguvu kabisa mfano: kupenda Kupongezwa kujidai wewe ni nabii wa pekee na hakuna duniani aliye kama wewe., kujivuna. Wengine wanatafuta kujulikana. Wengine wanapenda kutambuliwa na ulimwengu….N.k. Kumbuka unatumika na Roho Mtakatifu Aliyetumwa Na Mungu ili alifundishe kanisa na kuliweka katika kweli yote, uwe Mnyenyekevu na mpole. viii. Kuna baadhi ya manabii wameshikwa na tama ya kupenda Pesa kupita kiasi. Hili ni tatizo la hatari mno. Tuepuke tatizo hili. Badala yake Pesa zitutumikie sisi, Wala tusikubali zikatuingiza katika kusalimu amri, (moral compromise), au Kuzipigia magoti. Anayestahili kupigiwa magoti ni Yesu tu Aliye, Mwokozi wetu. Namna ya Kuupima Unabii: Unabii unapimwa kama ifuatavyo:- i. Vinywa vya mashaidi zaidi ya mtu m’moja: Inatakiwa watu kama watatu wawe mashahidi wa kuthibitisha unabii uliotolewa, ili kupata maneno ya kanuni na yaliyo ya hakika. Watu wa aina hii nilazima wawe wamejaa Roho Mtakatifu, na wamepevuka katika maneno ya kiroho. Kuwa mchungaji, au askofu na una shahada ya theolojia, haikupi sifa za kuupima unabii. Ukilazimisha, utaharibu kila neno. Na hivi ndivyo makanisa ya Afrika mashariki yalivyo poteza utukufu, baada ya kukimbiwa na Roho Mtakatifu, kulikosababishwa na kuutweza au kuuharibu unabii, kwa kutumia vyeo vyao na sio kuongozwa na Roho Mtakatifu. Na baadaye huduma ya unabii kupotea katika makanisa na huduma mbalimbali za walio okoka. 2Korintho13:1…”Hii ndio mara ya tatu mimi kuja kwenu. Kwa vinywa vya mashaidi wawili au watatu kila neno litathibitishwa”. ii. Omba upewe ishara yoyote ili na Roho Mtakatifu upate uhakika wa unabii ulioupokea; ili kupata uthibitisho wa uhakika. Waamuzi 6:35-37 … “Kisha akatuma wajumbe waende kati ya Manase yote wao nao walikutana pamoja ili kumfuata ; kasha akatuma wajumbe waende kwa Asheri na kwa Zabuloni na kwa Naftali, nao wakakwea ili kumlaki, Gideoni akamwambia Mungu ikiwa wewe utawaokoa Israeli kwa mkono wangu, kama ulivyosema, tazama nitaweka ngozi ya kondoo katika kiwanja cha kupuria, na kama ukiwapo umande juu ya ngozi tu, na nchi yote ikawa kavu, basi ndipo nitapo jua ya kwamba utawaokoa Israeli kwa mkono wangu, kama ulivyosema Waamuzi 6:40… “ Mungu akafanya vivyo usiku ule; maana ile ngozi tu ilikuwa kavu, napo palikuwa na umande juu ya nchi yote. iii. Kwakutumia mtumishi mwenye neema ya kuhudhuria baraza la mbinguni, ili kuhakikisha akiwa kule mbinguni kama ni kweli unabii huo ulitoka kwa Mungu au la ! Yeremia 23:18… “Maana ni nani aliye simama katika baraza la BWANA, hata akalifahamu neno lake na kulisikia ? ni nani aliyelitia moyoni neno langu , na kulisikia? iv. . Kwa njia ya andiko. Unaweza kutumia andiko katika kuupima unabii. Lakini peke yake hii haitoshi bila msaada wa karibu wa Roho Mtakatifu.( Yaani ufunuo wa Roho Mtakatifu)
Posted on: Thu, 15 Aug 2013 16:45:24 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015