TALLIT: Jewish prayer shawl Namshuku Mungu, nimebakisha miezi - TopicsExpress



          

TALLIT: Jewish prayer shawl Namshuku Mungu, nimebakisha miezi mitatu kumaliza miaka miwili ya kuwa darasani kwa masomo yangu kwa ngazi ya degree katika chuo cha “Christian Leadership University” . Wiki hii tulikuwa tunajifunza “The seven feast of Irael”, yaani sikuu saba za taifa la Israeli na umuhimu wake katika kizazi chetu. Pamoja na mengi niliojifunza ndani ya somo hilo la ajabu, nimevutiwa sana na somo la “The Jewish wedding” yaani utaraibu wa ndoa za kiyaudi tangu uchumba hadi harusi. Hapo utona picha ya kanisa na Bwana Harusi ambaye ni Yesu Kristo. Pia tumejifunza kuhusu lile vazi wanalolitumia wayaudi wakati wa kusali au kuomba (Tallit: Jewish Prayer Shawl). Ni kweli tunaongozwa na Roho Mtakatifu, Tunaifahamu sana mistari ya Biblia, lakini ushauri wangu kwa waimbaji wa Injili, wainjilisti, wachungaji na kwa kila mkristo, katika kizazi hiki cha sayansi na teknologia, kizazi chenye uovu wa kila aina; tunahitaji kukaa chini nakujifunza Neno la Mungu. Young Pastor
Posted on: Mon, 02 Sep 2013 09:57:02 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015