THIAGO ALCANTARA: “”MAN UNITED HAWAKUNIFUATA! NI MAGAZETI - TopicsExpress



          

THIAGO ALCANTARA: “”MAN UNITED HAWAKUNIFUATA! NI MAGAZETI TU! Friday, 26 July 2013 07:24 >>MOURINHO AMPA MOTO TORRES!! KIUNGO mpya wa Mabingwa wa Ulaya Bayern Munich, Thiago Alcantara, amesisitiza kuwa Mabingwa wa England Manchester United hawakuwahi hata Siku moja kumfuata ili ahamie Old Trafford. Alcantara, Miaka 23, hivi karibuni aliihama Barcelona na kutua Bayern Munich na kuzima uvumi kuwa Man United ilikuwa ikimtaka. Juzi Baba wa Alcantara, Mazinho, Mchezaji wa zamani wa Brazil ambae pia ni Wakala wa Kiungo huyo, alidokeza kuhusu Man United kuwa na nia ya kumchukua Mwanawe lakini Mchezaji huyo amepinga hilo. Thiago Alcantara ametamka: “Ukweli ni kwamba hamna hata wakati mmoja Man United walikuja kwetu na kuongea na sisi. Hayo yametoka kwenye Magazeti, Siku zote ni uongo!” Mourinho na Torres BOSI wa Chelsea Jose Mourinho anaamini Straika wake Fernando Torres atapendelea ushindani wa namba utakaokuwepo Klabuni hapo kwa Msimu ujao. Torres hakuwepo kwenye Kikosi cha Chelsea ambacho kilizuru Asia kwa vile aliongezewa likizo kwa kushiriki Kombe la Mabara na Spain huko Brazil lakini atajumuika na wenzake kwa safari yao huko USA Wiki ijayo. Kukosekana kwa Torres kulitoa mwanya kwa Romelu Lukaku, ambae Msimu uliopita alikuwa kwa Mkopo West Bromwich Albion, kung’ara na kupiga Bao katika Mechi zao. Sasa Mourinho amehakikisha Lukaku atabaki Stamford Bridge na hivyo kugombea namba pamoja na Demba Ba na Torres. Mourinho amesema: “Nadhani Torres atakuwa na furaha kwa sababu tuna ushindani katika kila namba na hili ni safi kwa kila Mtu! Sasa tuna Mastraika watatu!”
Posted on: Fri, 26 Jul 2013 05:47:22 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015