Tumeshangazwa mno na ukimya wa Serikali kuhusu janga kubwa la - TopicsExpress



          

Tumeshangazwa mno na ukimya wa Serikali kuhusu janga kubwa la biashara ya dawa za kulevya ambalo limeikumba nchi yetu kwa muda mrefu sasa. Hatutaki kuamini kwamba Serikali haina taarifa za kuwapo kwa janga hilo hapa nchini, wala kuamini kwamba Serikali hiyo bado haijatambua ukubwa wa tatizo hilo. Mbali na kauli nyepesi za polisi na taasisi nyingine husika kwamba zinafanya uchunguzi ili kugundua watu wanaojihusisha na biashara hiyo, hatujasikia kauli nzito kutoka kwa kiongozi mkuu wa nchi, Rais Jakaya Kikwete ambaye ndiye pekee mwenye sauti yenye mamlaka anayeweza kuzungumzia tatizo hilo, hasa kwa kutilia maanani kwamba biashara hiyo haramu sasa imefikia kiwango cha kutisha na wananchi wamechoka kusikia ahadi zisizotekelezeka za kuikomesha. Hivyo, wakati huu wananchi hawategemei Rais Kikwete atoe kauli zilizozoeleka kwamba anayo orodha ya watu wanaojihusisha na biashara hiyo na kuwataka waache uhalifu haraka. Tunasema kauli kama hizo zimezoeleka kwa wananchi na sasa ni wakati wa kuwaeleza hatua zilizochukuliwa dhidi ya watu hao, ikiw Read more: vitukovyamtaa.blogspot/2013/08/dawa-za-kulevya-na-ukimya-wa-serikali.html#ixzz2buLRpl1e
Posted on: Wed, 14 Aug 2013 02:47:30 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015