UCHUMI UNAPOROMOKA WANASIASA WANAONGOPA/ WENYE DHATI WACHACHE - TopicsExpress



          

UCHUMI UNAPOROMOKA WANASIASA WANAONGOPA/ WENYE DHATI WACHACHE WENGINE WANAROPOKA/ RAIA WANASOTA NJAA TUMBONI INAWASOKOTA/ WENGI MADHAMBI WANAJIFANYA WAMEOKOKA/ PEPO WANAIOTA MIPANGO YAO INAGOTA/ SASA WANAOKWA NA MOTO UNAOKOKWA/ WAMESHACHOKA JASHO LA DHIKI LINAWATOKA/ SIKU ZINAPITA MUNGU WANAMWITA WANAKOKOTWA/ KAMA MPIRA WA SOKA WENYE VYEO PESA WANACHOTA/ HURUMA HAWANA WAMESAHAU WALIPOTOKA/ KUPATA NI NYOTA ALIYE JUU ATADONDOKA/ NDO MANA VIJANA MALENGO YAO NI KUCHOMOKA/ NCHI HII KUITOKA INGEKUWA POA WASINGEONDOKA/ NASEMA UKWELI SIO UTAPELI WALA MAHOKA/ NSHAUMWA NA NYOKA NSHAKWENDA MBIO KAMA MOTA/ NAMBA HAIJATOKA AJIRA MBAWA IMEOTA/ NYUMBA SIMILIKI NAAMBIWA TOKA KWENYE KOTA/ NTAISHI VIPI HAKUNA PESA KUOKOTA/ MATOKEO WIZI ,UCHIZI NA KUPOTOKA/ HATA UKIENDA RESI VIPI BAHATI ZINAPONYOKA/ YUPI UTAMWOMBA NANI AKULAANI UKIMKOPA/ UTAMLIPA NINI KAZINI UMESHANGOKA/ HATA UWE WA SHOKA HALI HII UTAIOGOPA/ UBETI WA KWANZA MWISHO VITISHO MI NABOMOKA. SALU T. - HALI YA HATARI
Posted on: Thu, 28 Nov 2013 17:11:27 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015