Utoro maskulini ni miongoni mwa sababu zinazopelekea watoto kufeli - TopicsExpress



          

Utoro maskulini ni miongoni mwa sababu zinazopelekea watoto kufeli mitihani yao Na Abdi Suleiman, Pemba WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Ali Juma Shamhuna amesema kuwa, utoro kwa wanafunzi wengi skulini ni moja ya sababu kubwa, iliyopelekea matokeo mabaya ya mitihani kwa wanafunzi wa Zanzibar mwaka 2012. Waziri Shamhuna aliyaeleza hayo, huko katika kiwanja cha michezo gombani chake chake Pemba, wakati alipokuwa akiwahutubia walimu na wanafunzi mbali mbali katika maadhimisho ya miaka 49 ya elimu bila ya malipo Zanzibar. Shamhuna alisema kuwa, utoro kwa wanafunzi pamoja na walimu kutokumaliza mtaala wakufundishia wanafunzi pia kwa kiasi kikubwa kilichangia kupatikana kwa matokeo mabaya ya mitihani kwa wanafunzi mwaka 2012. Alisema kuwa, mitihani inayotungwa inatokana na mitaala inayotumiwa na walimu katika kuwafundishia wanafunzi, hivyo aliwataka walimu kuhakikisha wanamaliza mitaala yao katika kuwasomesha wanafunzi skulini. “Hili tulilibaini katika mikutano yetu tuliyoifanya kila mkoa kwa mikoa yote mitano ya Zanzibar, pale tulipokutana na walimu wakuu, kamati za skuli pamoja na baadhi ya wadau wa elimu, humo ndimo tulipopata taarifa hiyo’alisema. Akizungumzia suala la mishahara ya walimu, waziri Shamhuna alisema kuwa, Serikali imeandaa mpango mzuri kwa walimu wenye mafanikio, utakao pelekea kuwatunza walimu wake. Alisema kuwa bado serikali ineendelea na jitihada zake za kufundisha walimu wa masomo ya sayansi katika vyuo vyake vikuu, ili kuweza kuwa na walimu bora wa kisasa wa masomo ya sanansi ambao watakao weza kukidhi mahitaji ya wanafunzi. Aidha alisema bila ya kutokuwa na walimu bora, haiwezekani kutoa wanafunzi bora, hivyo walimu hawana budi kutimiza wajibu wao, kwa kuwafundisha wanafunzi kikamilifu ili kuweza kupata viongozi bora hapo baadae. “Zanzibar tuna vyuo vikuu vitatu ambavyo sasa vyote vinafundisha masomo ya sayansi kwa walimu, ili baadae waje waweze kuwafundisha ndugu zao na kuweza kukidhi mahitaji ya walimu wa somo hilo. Hata hivyo alisema kuwa, Serikali itaendelea na juhudi zake za kujenga skuli za kisasa zenye ubora zaidi, ambazo zitakazo weza kukidhi mahitaji ya wanafunzi ikiwemo vyumba vya maabara, vyumba vya kompyuta na mktaba ya vitabu vya kusomea. Akimkaribisha waziri wa elimu, mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Juma Kassim Tindwa, alisema kuwa walimu, wazazi na wanafunzi hawana budi kushirikiana ipasavyo ili kuhakikisha watoto wanapata elimu ipasavyo. Hata hivyo, aliitaka wizara ya elimu kuhakikisha inawachukulia hatua kali za kisheria, wale wote wanao wabaka watoto na kuwadhalilisha kijinsia pamoja na kuwakatisha masomo yao, ili iwefundisho kwa wengine. “Hapa kwetu Pemba hatuna budi kumpongeza hakimu Khamis Ramadhan Abdalla kwani hataki uzembe na wabakaji, tayari kesi tatu ameshazipatia hukumu, hii itakuwa fundisho kwa wengine”alisema Tindwa. Naye mkurugenzi wa elimu ya msingi, Uledi Juma Wadi alisema kuwa lengo la tamasha la elimu bila ya malipo ni kutathmini utolewaji wa kiwango cha elimu pamoja na vipaji vya wanafunzi kimichezo na utamaduni. Uledi alisema wananchi wa Zanzibar wanapata elimu bora bila ya kwenda masafa marefu ikiwa ni miongoni mwa matunda ya mapinduzi matukufu ya Zanzibar 1964. Katika risala ya wanafunzi ya mikoa mitano ya Zanzibar, iliyosomwa katika maadhimisho hayo, imeiyomba wizara ya elimu kufanya utafiti wa matokeo mabaya ya mitihadi ya wanafunzi, ili kugunduwa changamoto zinazosababisha kuwepo kwa matokeo mabaya ya wanadunzi wa kidatu cha nne na sita. Risala hiyo ilisema kuwa, wanafunzi wanapaswa kuwa mstari wa mbele zaidi katika masomo yao kwani ndio nguvu kazi ya taifa linalokuja. Hata hivyo risala hiyo imesema kuwa mwaka 1964 kulikuwa na skuli za msingi 62 na sekondari 734 na sasa kuna skuli za msingi 263 na sekondari 205 na skuli za maandalizi ni 34, ambapo sasa ni jambo la kujivunia. CHANZO:ZANZINEWS
Posted on: Wed, 25 Sep 2013 00:38:30 +0000

Trending Topics



le="min-height:30px;">
David & Micheal were lost in the Sahara desert. They were dying

Recently Viewed Topics




© 2015