hadithi ya kusisimua" MWANAMKE MWENYE KOVU JEUSI" SEHEMU YA - TopicsExpress



          

hadithi ya kusisimua" MWANAMKE MWENYE KOVU JEUSI" SEHEMU YA 1 ************************ ************************ ************************ Nakumbuka vizuri ilikuwa siku ya jumapili ambayo kama ilivyoada kwangu huwa sikosi kwenda kanisani hasa misa ya kwanza kwani huwa napenda sana kusali misa ya kwanza ili baadaye niweze kuendelea na mambo yangu mengine,siku hiyo niliamka asubuhi na mapema kutoka pale nyumbani kwangu mnazi mmoja karibia na ofisi za chama cha mapinduzi za mkoa wa Dar-es-salaam na kuelekea kanisani pale saint.alban posta taratibu kwa miguu kwani gari yangu ilikuwa imeharibika wiki ya pili sasa na isitoshe pale nyumbani kwangu mpaka pale posta hapakuwa mbali sana kiasi cha kama dakika 20 tu hasa kwa kijana kama mimi ambaye damu ilikuwa bado inachemka.niliingia pale kanisani nikiwa sijachelewa sana misa ilikuwa imeanza kama dakika 7 hivi nakumbuka sana somo la siku hiyo alilolitoa padri Kiaka lilikuwa linahusu umuhimu wa kuombea siku yako ya kufa kwani haina siku wala saa. Misa ilipoisha mida ya saa 3 asubuhi niliona nijivute mpaka mitaa ya upanga pale nyuma ya diamond jubilee mwendo wa pole pole nikamuone rafiki yangu Martin ambaye pia alikuwa ni mfanyakazi mwenzangu. Sikutaka hata kumtaarifu kwenye simu kwani simu yangu haikuwa na pesa pia nilijua kwa kuwa tuliahidiana jana kwamba kesho nikitoka kanisani nitaenda kwake basi haina shaka nitamkuta tu kwani pia Martin huwa sio mzururaji sana hasa mida ya asubuhi kama haendi kazini.Wakati naingia ndani kwa rafiki yangu kipenzi Martin nakumbuka ilikuwa ni mida ya saa 4 asubuhi mlangoni nilipishana na mdada wa makamo mweusi kiasi ambaye nakumbuka vizuri alikuwa amevalia dela la rangi ya kijani kibichi likiwa linamichirizi ya rangi ya zambarau na kwa ndani alikuwa amevaa suruali ya jeans ya rangi nyeusi huku kichwani akiwa amejifunga mtandio mweusi kufunika nywele zake nilimsalimia aliitikia haraka haraka huku akikwepesha sura yake na huku akionyesha ni mtu aliyekuwa na shauku ya kuondoka lile eneo haraka sana, mimi hata sikumjali nilijua atakuwa ni mmoja kati ya wasichana ambao alikuwa na uhusiano nao bwana Martin kwa kuwa rafiki yangu Martin alikuwa ni mtu aliyependa sana wasichana,nilifika mpaka pale alipokuwa amepanga Martin ilikuwa ni nyumba ya uwani akiwa amepanga chumba na sebule huku nyumba ya mbele kukiwa hakuna mtu hata mmoja aliyekuwa amepanga kwa maelezo yake ile nyumba ya mbele kulikuwa na mpangaji lakini amehama na sasa mwenye nyumba alikuwa yupo akiifanyia marekebisho tayari kwa kuingia mpangaji mwingine. Ile nimefika tu mlangoni nikakuta mlango upo wazi kitu ambacho kikawaida sio busara kuingia nyumba ya mtu bila kugonga basi nikajivuta pale mlangoni na kuanza kuugonga ule mlango hallow Martin hallow niligonga kama dakika tano bila kupata jibu lolote kutoka mule ndani ilinibidi nishangae kidogo kwa maana hata kama angekuwa msalani ni lazima angesikia ile sauti yangu na kwa nini akae kimya sikuamini kama alikuwa amelala wakati nimepishana na Yule dada anatoka chumbani kwake muda si mrefu,ikanibidi niingie tu ndani kama hayupo atanikuta mule mule nikimsubili, mungu wangu sikuamini nilipoingia pale sebuleni kwake nilikutana na michirizi ya damu kutoka pale sebuleni kuelekea chumbani kwake mh ikanibidi nipitilize haraka moja kwa moja kule chumbani kwake ile kuingia tu nikakutana na mwili wa Martin akinikodelea macho huku ukiwa umekakamaa huku pia ukiwa umegandana na damu na alama kubwa ya kisu kwenye shingo yake,nilimkimbila pale alipokuwa amelazwa na kumuangalia mungu wangu alikuwa tayari ameshakufa,nilifikiria pale haraka haraka ni kipi nifanye nikaanza kuitafuta simu yake mule ndani mpaka nikaipata nikawapigia simu polisi na kuwaeleza lile tukio sikutaka nijihusishe moja kwa moja na lile tukio ndio maana niliamua kutumia simu yake pia simu yangu nilikuwa bado sijaweka vocha kisha nikaanza kutoka nje kabla sijatoka nje ya chumba chake macho yangu yakatua kwenye meza ndogo iliyokuwa mule chumbani kwake mara nikakutana na karatasi imeandikwa kwa Wino Mwekundu “NILIYEMUUWA NI MIMI MWANAMKE MWENYE KOVU JEUSI” ITAENDELEA
Posted on: Fri, 12 Jul 2013 13:07:51 +0000

Trending Topics




© 2015