ﻳﻔﻨﻰ KUKINAI NI HAZINA ISIYOMALIZIKA ﺑﺴﻢ - TopicsExpress



          

ﻳﻔﻨﻰ KUKINAI NI HAZINA ISIYOMALIZIKA ﺑﺴﻢ ﺍﻟﻠﻪ ﺍﻟﺮﺣﻤﻦ ﺍﻟﺮﺣﻴﻢ Baada ya kumshukuru Allah kama anavyostahiki kushukuriwa , sala na salamu zimfikie Mjumbe wake Sayyidna Muhammad s.a.w. pamoja na sahaba zake na kila anayefuata njia yake . Waja wa Allah: Tambueni ya kwamba kukinai hakuko mbali na mtu au jamii yake , bali kumeambatana na maisha ya mwanadamu ambaye hataki umaarufu katika matendo yake , wala unyang’anyifu katika kutafuta rizki yake , na kutokana na haya kukinai ni kuridhika mtu kwa alichopewa na Allah , ikiwa ni kidogo atasubiri na ikiwa kingi atashukuru , na yanawezekana haya pale mtu atakapoweza kuyashinda matamanio ya nafsi na kuyawekea mpaka , anasema Allah Mtukufu: ﻭﻻ ﺗﻤﺪﻥ ﻋﻴﻨﻴﻚ ﺇﻟﻰ ﻣﺎ ﻣﺘﻌﻨﺎ ﺑﻪ ﺃﺯﻭﺍﺟﺎ ﻣﻨﻬﻢ ﺯﻫﺮﺓ ﺍﻟﺤﻴﺎﺓ ﺍﻟﺪﻧﻴﺎ ﻟﻨﻔﺘﻨﻬﻢ ﻓﻴﻪ ﻭﺭﺯﻕ ﺭﺑﻚ ﺧﻴﺮ ﻭﺃﺑﻘﻰ / . ﻃﻪ 131 : Wala usivikodolee macho yako tulivyowastareheshea baadhi ya watu miongoni mwao . Hivyo ni mapambo ya maisha ya dunia tu , ili tuwafanyie mitihani kwayo . Na riziki ya mola wako (akupayo kwa halali) ni bora mno na iendeleayo . Na amepokea Abu dhari Al-ghafariy radhi za Allah zimfikie amesema : nilimuambia Ewe Mjumbe wa Allah niusiye, akasema: ﺃﻧﻈﺮ ﺇﻟﻰ ﻣﻦ ﻫﻮ ﺗﺤﺘﻚ ، ﻭﻻ ﺗﻨﻈﺮ ﺇﻟﻰ ﻣﻦ ﻫﻮ ﻓﻮﻗﻚ ، ﻓﺈﻧﻪ ﺃﺟﺪﺭ ﺃﻻ ﺗﺰﺩﺭﻱ ﻧﻌﻤﺔ ﺍﻟﻠﻪ ﻋﻠﻴﻚ . Mtazame aliye chini yako na wala usimtazame aliye juu yako , kwani kufanya hivyo kutakuepusha na kuidharau neema ya Allah iliyo juu yako. Na katika mawaidha ya Ibnu Omar radhi za Allah ziwafikie amesema : ﻳﺎ ﺍﺑﻦ ﺁﺩﻡ ﻋﻨﺪﻙ ﻣﺎ ﻳﻜﻔﻴﻚ ، ﻭﺃﻧﺖ ﺗﻄﻠﺐ ﻣﺎ ﻳﻄﻐﻴﻚ ، ﻳﺎ ﺍﺑﻦ ﺁﺩﻡ ، ﻻ ﺑﻘﻠﻴﻞ ﺗﻘﻨﻊ ، ﻭﻻ ﺑﻜﺜﻴﺮ ﺗﺸﺒﻊ . Ewe mwanadamu! Unacho kinachokutosha, nawe unataka kitakachokutakabarisha , Ewe mwanadamu! Hutokinai kwa kidogo, wala hutoshiba kwa kingi . Ndugu Waislamu: Muislamu wa kweli ni yule aliyekinai nafsi yake na cheo chake katika hii dunia , kwani anajua kuwa yeye si chembe iliyopotea wala wingi uliotupwa , na anaimani juu ya ahadi ya Allah na rehma zake , kuwa hakumuumba kwa mchezo , na wala hakumuachia bure , bali rehma zake juu ya mwanadamu hazihesabiki , na fadhila zake hazina mpaka , na anaamini kuwa neema yoyote inatokana na Allah , na anaamini kuwa jambo zuri linatokana na Allah na jambo baya linatokana na nafsi yake mwenyewe , na akawa anayasema maneno haya ambayo hapo kabla aliyasema baba yetu Sayyidna Ibrahim Alayhi salam : ﺍﻟﺬﻱ ﺧﻠﻘﻨﻲ ﻓﻬﻮ ﻳﻬﺪﻳﻦ ، ﻭﺍﻟﺬﻱ ﻫﻮ ﻳﻄﻌﻤﻨﻲ ﻭﻳﺴﻘﻴﻦ ، ﻭﺇﺫﺍ ﻣﺮﺿﺖ ﻓﻬﻮ ﻳﺸﻔﻴﻦ ، ﻭﺍﻟﺬﻱ ﻳﻤﻴﺘﻨﻲ ﺛﻢ ﻳﺤﻴﻴﻦ ، ﻭﺍﻟﺬﻱ ﺃﻃﻤﻊ ﺃﻥ ﻳﻐﻔﺮ ﻟﻲ ﺧﻄﻴﺌﺘﻲ ﻳﻮﻡ ﺍﻟﺪﻳﻦ /. ﺍﻟﺸﻌﺮﺍﺀ 82-78 : Ambaye ameniumba na yeye ananiongoza, na ambaye ndiye anayenilisha na kuninywesha, na ninapougua, yeye ndiye anayeniponesha. Na ambaye atanifisha kisha atanihuisha, na ndiye ninayemtumaini kwamba atanisamehe makosa yangu siku ya malipo . Kwa hivyo anayetulisha na kutunywesha ni yeye Allah , na yeye ndiye anayetupatia usalama na amani , naye ndiye anayeturuzuku uzima na afya , inasimuliwa ya kwamba amesema Mjumbe wa Allah rehma na amani zimfikie : ﻣﻦ ﺃﺻﺒﺢ ﻣﻨﻜﻢ ﺁﻣﻨﺎ ﻓﻲ ﺳﺮﺑﻪ ، ﻣﻌﺎﻓﻰ ﻓﻲ ﺟﺴﺪﻩ ، ﻋﻨﺪﻩ ﻗﻮﺕ ﻳﻮﻣﻪ ، ﻓﻜﺄﻧﻤﺎ ﺣﻴﺰﺕ ﻟﻪ ﺍﻟﺪﻧﻴﺎ ﺑﺤﺬﺍﻓﻴﺮﻫﺎ . Atakayepambazukiwa mmoja wenu amesalimika katika nyumba yake , mzima wa kiwiliwili chake , anacho cha kukila , basi huwa kama kwamba amekusanyiwa dunia yote . Basi Ewe muislamu! Ridhika na kidogo kwani hivi karibu utaihama dunia na utawaachia wengine , chako ni kile ulichokila na kukimaliza na ulichovaa kikamalizika , au ulichokitanguliza kikabakia , na kitu hicho tu ndicho kilichohifadhiwa , ama kingine kitapotea , basi nini kikupacho kukimbia , hali ya kuwa sehemu yako ni ndogo tu , nenda taratibu Ewe mtafuta dunia , kwani rizki yako imeshagaiwa na ajali yako itafika , basi tosheka na ulichopewa ili usalimike na masuali . Imepokewa kutoka kwa Abdilah bin Amri kwamba Mjumbe wa Allah amesema : ﻗﺪ ﺃﻓﻠﺢ ﻣﻦ ﺃﺳﻠﻢ ، ﻭﻛﺎﻥ ﺭﺯﻗﻪ ﻛﻔﺎﻓﺎ ، ﻭﻗﻨﻌﻪ ﺍﻟﻠﻪ ﺑﻤﺎ ﺁﺗﺎﻩ . Amefaulu aliyesilimu , na ikawa rizki yake ya kutosha na Allah akamkinaisha kwa alichompa . Waja wa Allah : Hakika kutokinai kunaleta tamaa , na tamaa ni miongoni mwa sababu za hilaki ya mtu , na upungufu wa muruwa , kwani huwenda tamaa yake ikampeleka katika hatari , kama udanganyifu na uongo na kushuhudilia shahada ya uongo na kuchupa mipaka katika mambo ya dini , na kuna watu waliojidhulumu nafsi zao kwa kudhani kuwa kukinai ni kuridhika na hali duni au maisha ya udhalilifu na kutojitahidi kutafuta maisha mazuri na ikapelekea kuifisha ari ya maendeleo katika jamii na badala yake kufurahikia umasikini na njaa . Hakika maumbile ya mwanadamu yanaipenda dunia na wala haishibi , kwani imekuja hadithi ya Mtume s.a.w. kutoka kwa Ibnu Abbas r.a. kwamba Mjumbe wa Allah amesema kuhusu picha hii : ﻟﻮ ﺃﻥ ﻻﺑﻦ ﺁﺩﻡ ﻭﺍﺩﻳﺎ ﻣﻦ ﺫﻫﺐ ﻷﺣﺐ ﺃﻥ ﻳﻜﻮﻥ ﻟﻪ ﻭﺍﺩ ﺁﺧﺮ ، ﻭﻻ ﻳﻤﻸ ﺟﻮﻑ ﺍﺑﻦ ﺁﺩﻡ ﺇﻻ ﺍﻟﺘﺮﺍﺏ ، ﻭﻳﺘﻮﺏ ﺍﻟﻠﻪ ﻋﻠﻰ ﻣﻦ ﺗﺎﺏ . Lau mwanadamu angelikuwa na bonde la dhahabu , basi angelipendelea kuwa na bonde lengine , na wala halishibishi tumbo la mwanadamu ila mchanga , na Allah anamsamehe kwa anayetubia . Na lau mwanadamu angeliachiliwa kujisalimisha kwa matamanio yake na tamaa yake , basi angelikuwa hatari juu ya nafsi yake na jamii yake kwa ujumla , kwa hivyo imekuwa hapana budi kumuongoza katika misingi madhibuti . Umma wa Kiislamu: Uzuri ulioje kwa mtu anayeishi hali ya kuwa amekinai katika haya maisha , ameridhika kwa alichopewa na Allah , haimshawishi nafsi yake kunyang’anya haki za watu na wala hapeleki mkono wake katika kitu cha mtu , kwa hakika aliyekinai anahisi furaha juu ya umasikini wake , furaha ambayo haipati tajiri asiyekinai , na ni wajibu tufahamu kwamba kukinai ni utukufu na heshima , ama tamaa ni udhalilifu na uduni , na nafsi iliyokinai huwa imetulia na kusalimika . Na ni vyema tuelewe kuwa muislamu wa kweli ni yule aliyeridhika kwa alichopewa na Allah katika rizki na bahati , na hii ndiyo maana halisi ya kukinai ambako kumehimizwa na dini na kuamrishwa na mitume na kufuatwa na watu wema , kwa hivyo ajihadhari mtu asije akamkodolea macho aliye juu yake kwa utajiri alonao , kwani hicho ni kitu kinachopita kisha kutoweka , na isijekupelekea kumuonea husda kwa yule aliyeneemeshwa na allah , kwani hiyo ni fadhila yake humpa amtakaye , na huwezi kujua wapi ipo kheri , kwani huwenda utajiri ukawa fitna na hatimae kuwa nakma , anasema Allah Mtukufu : ﺇﻧﻤﺎ ﺃﻣﻮﺍﻟﻜﻢ ﻭﺃﻭﻻﺩﻛﻢ ﻓﺘﻨﺔ ﻭﺍﻟﻠﻪ ﻋﻨﺪﻩ ﺃﺟﺮ ﻋﻈﻴﻢ / . ﺍﻟﺘﻐﺎﺑﻦ 15 : Bila shaka mali zenu na watoto wenu ni mtihani , na kwa Allah kuna ujira mkubwa kabisa . Basi mcheni Allah ndugu waislamu na jifunzeni kukinai katika mambo yenu kwani kukinai ni hazina isiyomalizika
Posted on: Sat, 24 Aug 2013 20:23:01 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015