Asalaam Alaykum ((Sifa ya Mtume [S.A.W])) Mwenyezi Mungu amesema - TopicsExpress



          

Asalaam Alaykum ((Sifa ya Mtume [S.A.W])) Mwenyezi Mungu amesema kumhusu Mtume S.A.W,sifa yake: "Bila shaka mnao mfano mwema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu 33:21 Amesema Abul Abbas Al-Mubarrad(R.A) (mfalme) kisra alizigawa siku zake,akasema:siku ya upepo inafaa kwa kulala,na siku ya mawingu ni siku ya kuwinda,siku ya mvua ni siku ya pumbao na kunywa na siku ya jua ni siku ya kutafuta haja(maisha);yaani ni siku ya kuhangaika". Lakini Mtume wetu Rehema na amani zimshukie-aliugawa mchana wake sehemu tatu;sehemu ya Allah,sehemu ya Ahli zake na sehemu ya nafs yake kisha tena akaigawa ile sehemu ya nafs yake baina ya watu,basi akawa akitaka msaada kwa kilicho chake juu ya kukidhi haja za watu na akisema: "Nifikisheni haja/shida ya yule asiye weza kunifikishia,kwani hakika Mwenye kuifikisha haja ya asiye weza kuifikisha mwenyewe,Allah atampa amani katika siku ya fazaa kubwa. Nasi hatuna budi ila kufwata Mwenendo wake aliyokuwa nao na ambao tumetakiwa kufwata-sunna yake.
Posted on: Mon, 24 Jun 2013 18:31:26 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015