Mtabiri Maalim Hassan NYOTA YAKO LEO ALKHAMISI TAREHE - TopicsExpress



          

Mtabiri Maalim Hassan NYOTA YAKO LEO ALKHAMISI TAREHE 18/7/2013 KAA - CANCER (JUN 22- JUL 22) Uzoefu wako hauwezi kukusaidia kufikia maamuzi katika mambo ya maendeleo, ni lazima kuwashirikisha wengine SIMBA - LEO (JUL 23 –AUG 22) Taarifa unazoendelea kuzihodhi zitakuletea matatizo, huu ni wakati wa wewe kuwa muwazi katika mambo yako kama unataka kufanikiwa. MASHUKE - VIRGO (AUG 23- SEPT 23) Washirika wako na watu wako wa karibu watakutisha kutokana na taarifa watakazokupa kukuhusu wewe, lakini hayo yasikusumbue akili endelea na mipango yako MIZANI - LIBRA (SEPT 24- OCT 23) Jaribu kuwa karibu na ndugu zako au watu wanaokuzidi umri hali hiyo itakuongezea nafasi ya kuwa na mafanikio katika maisha yako. NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22) Kuna watu wanatengeneza mazingira mabaya ya kukuharibia mambo yako, shikilia msimamo wako na usikubali kuyumbishwa utakwama. MSHALE - SAGITARIUS ( NOV 23 - DES 21) Siku ya leo kila mmoja ataonekana kupendezwa na wewe, hali hii inaweza kukufanya kuanguka kwenye caguo baya, unatakiwa kuwa makini. MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN 20) Leo Kuna mambo hautaweza kuyafanya peke yako ni lazima kuomba msaada kwa wengine, bila hivyo utaendelea kukwama. NDOO –AQUARIUS (JAN 21 – FEBR 19) Hisia zako zinaonekanakuwa na nguvu kuzima hali ya khofu, lakini uwezo unakosekana kwa sbabu ya kutokujiamini. SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20) Leo ni bora ukadharau mipango yote iliyokunyima nafasi awali, mpenzi au rafiki wa karibu anaweza kuwa msaada kwako. PUNDA- ARIES (MACH 21- APR 20) Maamuzi unayolenga kuyatoa yanaonekana kuegemea upande mmoja, wengine wanaweza kujenga chuki kwako wape nafasi. NG’OMBE – TAURUS (APR21 – MAY 20) Leo inawezekana ukashindwa kumuelewa mwenzako kwa sababu ya kuwa naye mbali, huu ni wakati muafaka wa kuwa naye karibu MAPACHA - GEMINI (MAY 21- JUN 21) Yaliyokutokea jana hayawezi kufanana na yale ambayo yatakutokea leo, kwa hivyo kama ulikwama au kama hukufanikiwa, jana leo jaribu tena mambo yanaweza kuwa mazuri.
Posted on: Thu, 18 Jul 2013 06:00:16 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015