RWANDA YAMJIBU RAIS KIKWETE Serikali ya Rwanda imetoa tamko - TopicsExpress



          

RWANDA YAMJIBU RAIS KIKWETE Serikali ya Rwanda imetoa tamko linaloonyesha kutoielewa kauli ya Rais Jakaya Kikwete, iliyoamuru wahamiaji haramu kuondoka nchini, hali inayoonekana kukwepesha hoja. Rwanda kupitia waziri wake wa Mambo ya Nje, Louise Mushikiwabo, ilikaririwa ikieleza kwamba hawatajibu mapigo agizo la Rais Jakaya Kikwete ya kuwataka Wanyarwanda wote waliolowea Magharibi mwa Tanzania kuondoka haraka. Mushikiwabo alisema wako tayari kuwapokea na kuwalinda wote waliofukuzwa Tanzania kwa kisingizio kuwa ni wahamiaji haramu, akieleza kwamba anasikitishwa kwa kuwa Tanzania haikufanya jitihada yoyote kuwasiliana na Rwanda kuhusu suala hilo kabla ya kuchukua uamuzi huo. “Ni uamuzi ambao umeshachukuliwa, hatukushirikishwa kwa namna yoyote na jukumu letu kama serikali na taifa ni kuwahakikishia ulinzi wote wanaokuja, na hili ndilo suala tunalolishughulikia kwa sasa,” alisema. Rais Kikwete wakati akihitimisha ziara yake mkoani Kagera alitoa agizo la kuwataka wanaomiliki silaha kinyume cha sheria na wahamiaji haramu ama kuondoka au kuhalalisha ukazi wao, huku akitoa wiki mbili kwa zoezi hilo kutekelezwa, kabla ya kuanza kwa operesheni ya kuwasaka watu hao. Kauli hiyo ilitokana na kushamiri vitendo vya kihalifu katika eneo la Kanda ya Ziwa, Rais hakutaja jina la nchi ya wahamiaji hao. Kwa ukanda huo Tanzania inapakana na Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na DRC. Source: Mwananchi
Posted on: Sat, 10 Aug 2013 09:48:50 +0000

Trending Topics



e="min-height:30px;">
I am over the bandwagon of burning jerseys, taking them off
How to Find FLU Designs F-35004 Grip Seat Cover for YZ 125/250
ျမန္မာျပည္ MOH
Oooops having promised myself I was not going to get another pup
Out of love, theres nobody around All I hear is the sound of a
I feel at this time I can share a little about the progress Zac

Recently Viewed Topics




© 2015