Rais wangu, kila nchi ina wendawazimu wake. Hata hapa kwetu tunao - TopicsExpress



          

Rais wangu, kila nchi ina wendawazimu wake. Hata hapa kwetu tunao wetu. Wakati wewe kwa kutumia busara zako unawaita Wapinzani waje ikulu kwa majadiliano muhimu, hawa wa kwetu wamesikika wakipingana na wewe. Wanasema milango ya Ikulu imefungwa! Utadhani yeye ni bawaba za milango na madirisha ya Ikulu au ni bawabu wa lango kuu la kuingilia Ikulu. Haikubariki mtu tu apingane na kauli ya Rais wangu. Uhuni wa viongozi wa aina hii ndio huifanya serikali yoyote ionekane ya kihuni popote! Tusikubali uwendawazimu wa wachache uichafue serikali yetu. Baba waondoe hawa mapema wananchi wasije wakakufananisha nao. Muda wa matumizi wa ubongo wao kufikiri ‘ume-eksipaya’, wanapaswa waondolewe! CHANZO: TANZANIA DAIMA
Posted on: Wed, 09 Oct 2013 14:49:58 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015