COCOJAMBO ASUBUHI HII: JUMATATU, 18.11.2013: (HABARI). Zanzibar - TopicsExpress



          

COCOJAMBO ASUBUHI HII: JUMATATU, 18.11.2013: (HABARI). Zanzibar inaanza kuonja makali ya mgao wa umeme utakaodumu kwa muda wa siku 8 saa 24 kwa siku katika mgawanyo wa zone tofauti. Wakaazi wa maeneo ya Makadara na Kikwajuni, wamelalamikia uwepo wa ngoma za kibuki katika maeneo yao. Aliekuwa mke wa Nelson Mandela,Winnie Madikizela amesema kuwa Nelson Mandela sasa ni mgonjwa sana na hawezi kuzungumza. Misaada ya kimataifa imeanza kuonyesha dalili ya kupatikana unafuu katika kisiwa cha Ufilipino kilichokumbwa na maafa ya kimbunga Haiyan siku tisa zilizopita. FRANCE wako tayari ‘kufa’ ili kufanikiwa kucheza Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil Mwakani wakijaribu kupindua kipigo cha 2-0 walichopewa na Ukraine Ijumaa wakati watakaporudiana Jumanne Stade de France Mjini Paris kwa mujibu wa Straika wa France, Olivier Giroud, anaechezea Arsenal. MAONI: +255 772 389889.
Posted on: Mon, 18 Nov 2013 04:33:24 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015