COCOSPORTS USIKU HUU: IJUMAA, 23.08.2013: (Saa 2 kamili - TopicsExpress



          

COCOSPORTS USIKU HUU: IJUMAA, 23.08.2013: (Saa 2 kamili Usiku). Mafunzo kwa Waamuzi watakaochezesha Ligi Kuu Visiwani Zanzibar yamefungwa aubuhi ya leo na Mkufunzi Lisle Liunda. MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Vodacom, Yanga, ambao wamekuwa katika matayarisho kamambe na wanaaza utetezi wao Jumamosi Agosti 24 Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kwa kucheza na Ashanti United, iliyopanda Daraja Msimu huu, wamesema wako tayari kwa kampeni yao. Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imebandika rasmi kwenye ubao wa matangazo majina ya waombaji uongozi kwenye uchaguzi wa TFF na Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board) ili kutoa fursa kwa pingamizi. Tiketi za elektroniki zitaanza kutumika katika mzunguko wa nne wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) utakaoanza Septemba 18 mwaka huu. Tayari benki ya CRDB ambayo ndiyo ilishinda tenda hiyo imeshakamilisha ufungaji wa vifaa kwa ajili ya matumizi ya tiketi hizo katika viwanja vyote. Klabu ya Manchester City imempeleka mshambuliaji wake,Scott Sinclair katika klabu ya West Brom kwa mkopo wa muda mrefu. Kocha wa klabu ya Arsenal,Arsene Wenger amejipanga kupeleka ofa kwa Real Madrid kwa ajili ya kuwanasa wachezaji wawili wa klabu hiyo ya Uhispania Karim Benzema na Angel Di Maria. KINDA wa Miaka 16 tu alieingizwa kwenye Kikosi cha Klabu maarufu Brazil Santos Dakika zaGABIGOLmwisho kabla Mechi yao ya Robo Fainali ya Copa do Brasil dhidi ya Gremio hapo Jana aliingizwa kwenye Mechi hiyo Kipindi cha Pili na kufunga Bao pekee na la ushindi katika Dakika ya 82 na kuipa Santos ushindi wa Bao 1-0. VETERANI wa Manchester United Rio Ferdinand anaamini Mechi za Timu yao dhidi ya Liverpool na Manchester City ndio ‘BIGI MECHI’ kupita Chelsea ambao watawavaa Jumatatu Usiku Old Trafford kwenye Mechi ya Ligi Kuu England.
Posted on: Fri, 23 Aug 2013 16:28:13 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015