HILI LA WATOTO WA MITAANI LIMETUSHINDA. As published on Fahamu - TopicsExpress



          

HILI LA WATOTO WA MITAANI LIMETUSHINDA. As published on Fahamu Newspaper 17/09/2013 Dear CHILDREN STAKEHOLDER. .........IMMEDIATE EFFORTS TO SAVE STREET CHILDREN IN TANZANIA.It is more risk than the way we take it. The attached article was published on Fahamu weekly newspaper(Tanzania) Sept 17,2013. The article reveals how we jeopardize our today and next nation by keeping the fast growing of street Children in our nation Tanzania. I wrote this aiming to ignite the will and efforts to fight the problem among Tanzanians and I hope you are one of them.Sorry as it is in Swahili only but the English version is will be ready soon. LA WATOTO WA MITAANI LIMETUSHINDA?...BAADAE TUSIJEKIMBIANA. Tatizo la watoto wa mitaani Tanzania lishakuwa kama donda ndugu ambalo kila mtu na hata mwenyenalo analitazama na kuziba pua yake ili asisikie harufu ya uvundo wake huku akiendelelea kulitazama likimwangamiza. Hivi sasa tunasikia malalamiko ya madereva wa magari kuhusu bughudha wanazopata kutoka kwa watoto ombaomba wakiwa kwenye foleni za hapa Dar es Salaam hao ni wale tunaowaona tu barabarani na vituko vyao.Vipi kuhusu wale ambao hawako barabarni ila wanazunguka kwenye viambaza vya majumba na mitaa.Je, tunajua nini wanafanya na kufanyiwa? na mustakabali(taswira) wa hili kwa taifa lijalo la Tanznaia itakuwaje? Takwimu zilizotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF) kwa kushirikiana na Shirika la Kazi Duniani (ILO) zinaonyesha kuwa watoto wa mitaani duniani wanakadiliwa kufikia milioni 120, milioni 30 kati ya hao wako barani Afrika.Na kwa mujibu wa shirika lisilo la kiserikali la Global Giving limeinisha kuwapo kwa watoto wa mitaani zaidi ya 437,500 Tanzania nzima.Wakati huohuo Dar es Salaam pekee wamezidi kuongezeka kutoka3000 mika michache iliyopita hadi kufikia zaidi ya 6000 sasa. Kiuhalisi watoto hawa wamitaani si kwamba walizaliwa na mitaa kwa maana wazazi wao kuwa barabara na kuta za nyumba bali walizaliwa na binadamu ambao ama wazazi wao wako hai au washafariki.Swali la msingi hapa ni kwa nini wako mitaani .Watafiti mabalimbali wamechunguza uwepo wa wataoto hao kuwa ziko nyingi na miongozi mwao ni pamoja na zifuatazo:- Umaskini ambao unafanya wazazi wao washindwe kuwapatia huduma muhumu na hatimae wao wenyewe kuamua kwenda kuzitafuta kwa kuombaomba mtaani.Mfano watoto wengi wanaozunguka kwenye barabara za Dar es Salaam maeneo ya Posta, Moroko na Kariakoo wametoka mikoa mablimbali ya Tanzania kama vile Dodoma na kwingineko. Umaskini huu pia husababishwa na wazazi kutengana hasa pale baba anapomwacha mama na kumwachia mama jukumu la malezi.Wapo wanawake ambao wanaoamua kuwatumia watoto wao kama kitegauchumi wa kwenda kutafuta fedha kwa kuombaomba barabarani.Utafiti uliofanywa na Shirika lisilo la kiserikali la Consortium for Street Children mwaka 2009 unaonesha kwamba njaa na umaskini vinabeba 35%, ya vichochezi vya watoto wa mitaani. Chanzo kingine ni pamoja na ukatili wanaofanyiwa watoto kutoka kwa wazazi ama walezi wao.Hivyo watoto hao wanaamua kukimbia mateso na kwenda kuishi popote watakapoana hawatapata mateso. Kwa mujibu wa ripoti ya UNICEF ulibaini kwamba zaidi ya 75% ya vijana wa kitanzania walikiri kufanyiwa ukatili wa kimwili wakiwa watoto na 25% walifanyiwa ukatili wa kihisia enzi za utoto. Kwa mujibu wa utafiti wa shirika la Consortium for Street Children ukatili dhidi ya watoto unachangia kuwepo kwa asilimia 50 za watoto wanaoishi mitaani ili hali ukosefu wa upendo kwa watoto unachangia kwa asilimia 11% na kuvunjika kwa familia kunachangia kwa asilimia 4. Kwa mujibu wa utafiti huu sababu kubwa bila kudharau sabau zingine ni Ukatili namanyanyaso wanaofanyiwa watoto.Tafsiri yake ni kwamba tuliowengi katika jamii ya kitanzania hatujajenga hulka ya kuwa na urafiki na upendo kwa watoto.Pia hatujali haki za watoto na hata kuwafnya kama punda.Hatuna namna nzuri ya kumwadabisha na kumwelimisha mtoto.Pi katika hili jamii bado haijatambua jukumu la kumlinda mtoto na ndio maana kila kukicha utasikia visa vya ukatili kwa watoto. Umaskini na njaa vimechukua namba mbili.Kwa tafsiri rahisi tuseme mtoto kushindwa kupata huduma na mahitaji yake ya msingi.Hivyo tutegemee maeneo mengi yenye umaskini na ukatili kwa watoto yatazalisha watoto wengi wa mtaani.Tatizo la umasikini lishakuwa mwiba kwa nchi yetu limekuja na mambo mengi sana ila nataadharisha sana tusichukulie umaskini kwa vile ni miongoni mwa vyanzo viikuu na tatizo la wengi Tanzania basi tukabweteka na kudhani kwamba ni ngumu sana kukabiliana na wimbi la ongezeko la watoto wa mitaani. Tatizo la watoto wa mitaani linawakera wengi ila suala linakuja namna ya kuakailiana nalo kutoakana na uzito wa vyanzo vya tatizo lenyewe na kukosa nia ya dhati kutoka kwa jamii ya kupambana na tatizo lenyewe.Matokea yake kila mtu anasubiria mtu mwingine aje kutatua tatizo hili. Kumekuwa na harakati kadha wa kupambana na tatizo lenyewe ambazo bado si madhubuti sana katika kukabiliana na kutatua kabisa tatizo la watoto wa mitaani. Hivi karibuni serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto ameitaka mikoa yote ya Tanzania kuandaa mipango maalumu kwa ajili ya kuwarejesha watoto hao wa mitaani katika familia zao na pia waziri Simba mhusika wa wizara hiyo aliitaka serikali kuandaa bajeti zaidi kwa ajili ya kudhamini mahitaji ya watoto wa mitaani. Kwa mujibu wa ripoti ya serikali ya mkoa wa Dar es Salaam kwenye tovuti yao wanaseama “Mkoa umeendelea kusimamia na kutekeleza sheria na mikataba mbalimbali ya Kimataifa iliyoridhiwa na Serikali kuhusu haki na ustawi wa mtoto. Utekelezaji katika eneo hili unafanyika kwa ushirikiano na wadau mbalimbali.Mafanikio..65,000 wameshiriki katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto Duniani ambayo hufanyika mwezi Juni ya kila mwaka. Kila Halmashauri ya Manispaa imeunda baraza la watoto lenye wajumbe wasiozidi 60 kwa ajili ya kujadili masuala ya maendeleo.Watoto13,468 wanaoishi katika mazingira magumu wakiwemo wasichana 6,050 na wavulana 7,418 wametambuliwa,Kamati 158 zimeundwa ngazi ya mtaa ili kushughulikia matatizo ya watoto waishio katika mazingira hatarishi.Aidha kamati hizo zimepatiwa baiskeli 916 ili kurahisisha utendaji kazi.” Swali la kujiuliza uhalisia wa utekelezwaji wa haya yote pamoja na kamati zote zinazoundwa yako wapi ama ndio yale mambo yakuandikwa kwenye karatasi kisha yatajitekeleza yenyewe? Mwaka 2006 serikali chini ya ufadhili wa Umoja wa Mataifa ilianzisha Mpango kazi wa Taifa kwa watoto walio kwenye uwezekano wa kuathirika.Kwa mujibu wa taarifa zilizo kwenye vyanzo mabalimbali vya habari tarehe 1 Septemba mwaka huu serikali kwa ufadhili wa Shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia watoto(UNICEF) imenzisha progarmu ya kuchukua watoto wasio na makazi zaidi ya 3,000 katika mitaa ya Dar es Salaam na kuwarejesha nyumbani , ambao utatoa malazi ya muda kwa watoto wasio na makazi maalumu kuwapeleka shule, na kuwaunganisha na wazazi wao au wanafamilia.huu ni mwendelezo wa Mpango wa Taifa ulioanza mwaka 2006. Kwa mujibu wa Monica Mwaikenda, mmoja wa wafanyakazi wa huduma za jamii anayeshiriki katika programu hiyo.Katika awamu ya kwanza, serikali itawaondoa watoto wote katika mitaa na kuwaweke penye malazi mwishoni mwa mwezi huu na awamu wamu ya pili, ambayo itaendelea hadi mwishoni mwa mwaka huu, itahusisha kuwaunganisha na familia zao. Ukiangalia program hii inayolenga watoto 3000 pekee bado haifui dafu kukabiliana na tatizo la watoto ambao wanaongezeka siku hadi siku.Bado kunahitajika mpango uliosukwa kutokea kwenye jamii yenyewe ambacho ndio chanzo cha watoto wa mitaani. Sina uhakika kama serikali inatakwimu sahihi za idadi ya watoto wa mitaani kwani wakati wa siku ya mtoto wa Afrika Juni 16 serikali kupitia waziri wake ilitangaza kuazimia kufanya utafiti ili kubaini idadi ya watoto waishio mitaani na katika mazingira magumu, ambapo sanjari na hatua hiyo ipo katika mpango wa kutenga bajeti maalum kwa ajili ya watoto hao. Kuchukulia mzaha Tatizo la watoto wa mtaani hakufai hata kidogo.Fikiria jinsi watoto hawa wanavyoishi wenyewe huko mitaani na utawala wa serilai yao wenyewe.Fikiria ambavyo wanajiongoza wenyewe kwa akili zao za kitotoa na wengine kufundishwa maisha na watu wazima wasio kuwa na maadili. Mara nyingi watoto hawa hulala maeneo ya viambaza vya maduka,masokaoni n.k haya ni maeneo ambayo pia hata watu wazima wasiokuwa na makazi ambapo baadhi yao hujiusisha na utumiaji wa madawa ya kulevya hushinda na kulala.Si haba kwamba hata hawa watoto watakuwa wakifundishwa vitendo hivyo viovu,kama vile utumiaji wa madawa ya kulevya ,wizi ,uchangudoa na wengine kulawitiwa na kubakwa. Kama tutaacha idadi ya watoto wa namana hii waendeleee kuwepo na kuongeza lazima yujue kwamba hawa ndio watakuwa vijana wa Tanzania ya kesho,baba na mama wa Tanzania ya kesho na viongozi wa Tanzania ya kesho zaidi bila kusahau wahalifu waliokubuhu wa Tanzania iliyoko mbele yetu. Tuombe Mungu sana wahalifu wasije wakaanza kuwatumia kutekeleza mambo yao ya kihalifu kama jinsi wanavyotumika kwenye shughuli za kivita katika mataifa mbalimbali Afrika.Kwa mfano baadhi yao hivi sasa walioamua kujitengenezea ajira ya kuosha vioo vya magari yakiwa kwenye foleni,na akiosha ukagoma kumlipa atapaka gari lako vumbi ama kumwaga mapovu kwenye kioo cha gari,ushawahi kufikia vipi watoto hawa wakianza kutumia silaha,atapona mtu? Waswahili wanaseama mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.Watoto wa mitaani tukiendelea kuwaacha waongezeke tujue kwamba tunatengeneza tabaka la jamii ambayo imezoe kuishi huru kupita kiasi,yenye kila mtu na utawala wake,isiyojua kama duniani kuna upendo tena tabaka la watu waliozoea kuisha kwa machungu na kufanya lolote atatako bila kujali kuna mkubwa zaidi yake ama la. Ni tabaka amablo kupigana vita na kupindua serikali itakuwa ni kazi rahisi sana tena muda wowote wanapojisikia serikali inawabana na wanahisi kuichoka.Hili ndilo tunalolitengeneza leo. Suluhisho lake halifanywi na mtu mmoja bali kila mtu abebe jukumu analoweza kufanya mahali alipo.Mfano leo hii jirani zako(mume na mke) wanaweza wakagomabana tukawaacha lakini kumbuka wakitengana watoto wao wanaweza kuwa watoto wa mitaani.Tunapokuwa na watu kwenye jamii hawataki kufanya kazi wala kujishughulisha tunawatizama tu badala ya kuwahamasisha wafanye kazi ili wasishindwe kulea familia zao na kuiachia mitaa ilee. Lazima tufuate uzazi wa mpango,na sio kuzaa idadi kubwa ya watotot ambao mwisho wa siku unashindwa kuwalea.Nayo serikali inaposhindwa kutimiza wajibu wake wa kujenga fursa za kupambana na umaskini tunachukulia poa bila kuchukua hatua zozote watanznaia lazima tuanz e tabia ya kuiwajibisha serikali inaposhindwa kutekeleza majukumu yake.Taasisi za kushughulikia matatizo ya watoto hayatimizi wajibu wao ipasavyo tunayatizama bila hata kusema neno. Lazima jamii tuamue sasa kila mtu abebe wajibu wake.Na si kuridhika n ash 200,500 am 1000 tunazowapatia huko barabarani kwenye foleni.Zaidi sana ni kuwavutia waje kwa wingi kwani wanajua peasa zipo.Matokeo ya kupuuzia hali hii ni kutengeneza tabaka la kizazi ambacho hapo baadae tutatafutana. MWISHO Silas Bwire Children Stakeholder +255 655 66 00 30 Dar es Salaam,Tanzania. bwirebs2008@yahoo
Posted on: Thu, 19 Sep 2013 11:52:34 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015