KUIENZI LUGHA YA KISWAHILI 1. Nashangazwa na mwenendo, wa hawa - TopicsExpress



          

KUIENZI LUGHA YA KISWAHILI 1. Nashangazwa na mwenendo, wa hawa wetu Vijana, Niwachunguzapo nyendo, lughayo haina vina, Tutafika huu mwendo, Kiswahili kinachina?, Kiswahili lugha yetu, tuienzi kwa vitendo. 2. Nasema Watanzania, hata Kenya na Uganda, Kwa lugha hawana nia, kaulize hata Rwanda, Burundi wamehunia, kama wale wa Kiganda, Kiswahili lugha yetu tuienzi kwa vitendo. 3. Tunapoongea ‘Mombo’, hakika hatupendezi Kilikotoka ‘Kimombo’, wanatuona machizi, Twongeapo ‘Yombo Yombo’, tunawatoa machozi, Kiswahili lugha yetu, tuienzi kwa vitendo. 4. ‘Ck’ sasa ndio siku, Habari gani ‘niaje,’ Twapelekana mkuku, uharibifu uloje, Fesibuku nako huku, weledi sasa na uje, Kiswahili lugha yetu, tuienzi kwa vitendo. 5. Tamati nimefikia, kwa leo tano zatosha, Welevu watasikia, nasaha zitawatosha, Usomapo pata nia, makosa kurekebisha, Na Afrika mashariki, Kiswahili songa mbele Msamiati kuchina = kuharibika Kimombo = Kiingereza Yombo Yombo = hovyo hovyo mkuku = mwendo kasi Wasalaam, Mwana wa Elisamia, wa Andrea Msechu Dar es salaam, Tanzania.
Posted on: Tue, 01 Oct 2013 15:06:30 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015