Story: ZAWADI YA MOYO WANGU sehemu ya:8 siku zilikatika huku - TopicsExpress



          

Story: ZAWADI YA MOYO WANGU sehemu ya:8 siku zilikatika huku salome akizidi kupata mzuka wa kukutana na mtu ambae hakujua kuwa mtu anae mtafuta alikuwa anamuwinda yeye pia. Mbona sikutani nae? Aliwaza salome. Leo itabidi nitoke mapema. Ili ikiwezekana nitembelee sehemu nyingi tofauti tofauti. Salome alifika katika grocery moja hv akakaa akinywa kinywaji alichoagiza , kabla hajaenda sehemu aliyowaza aende kwa siku ile. richard wakati anangoja giz liingie vizuri aanze ratiba ya kuwaua wabaya wake alifika ktk grocery moja hv. Akawa amekaa hapo anakunywa. Ghafla aliingia msichana mmoja hv na kwenda kukaa jirani na alipo yeye. Mmmmh aliguna richard. Mbona haya majanga tena! Aliongea richar moyoni mwake. Alipo muona yule msichana mapigo ya moyo yaliongezeka kasi. Mwili ukasisimka. Alijishangaa imekuwaje! Kwa mala ya kwanza alihisi kuvutiwa na msichana kimapenzi. Alihisi kama vle roho yake ikimpata msichana huyo anaweza hata akaghairisha zoezi lake la kuua wanawake. Hakujua kuwa yule ndie salome itaendelea saa 3
Posted on: Fri, 26 Jul 2013 21:29:17 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015