TAARIFA KUHUSU TAMASHA LA KUCHANGIA WAGONJWA WA - TopicsExpress



          

TAARIFA KUHUSU TAMASHA LA KUCHANGIA WAGONJWA WA KANSA LILILOFANYIKA JANA JUMAPILI 30/6/2013 PALE VIWANJA VYA SINZA STAR JIJINI DAR ES SALAAM. Kwanza MUNGU Ashukulie Kwani mwamko kwa watu ulikuwa mkubwa zaidi, Kuanzia saa 5 Watu walianza Kuingia UWANJANI Hadi ilipofika Saa 8 Umati wa watu ulikuwa Mkubwa sanaa. MCHEZO WA REDE KWA AKINA DADA. Ilipofika Saa 8:45 mchana Wadada wazuri Wa Team ya FACEBOOK na Wadada Wa Team MEDIA walikuwa tayari Uwanjani kwa ajili Ya Mchezo huo Na ilipofika Saa 9:25 ulikwisha kwa TEAM Facebook Kuibuka na Ushindi wa Goli Moja kwa Sifuri. SAA 9:30 ULISOMWA MUKHTASARI KWA MGENI RASMI. MCHEZO WA FOOTBALL KWA WANAUME. Ilipofika Saa 9:45 Wachezaji wa Timu Media na Timu FACEBOOK walianza KUJIANDAA Kwa ajili ya Mechi kali. SAA 10:00 TAYARI VIJANA WOTE WA PANDE ZOTE MBILI WALIKUWA UWANJANI, FILIMBI ILIPULIZWA KUASHIRIA MCHEZO UANZE...! KULIKUA NA UPINZANI WA HALI YA JUU PANDE ZOTE MBILI, KILA TEAM ILIKUA IKITAKA USHINDI ILA TEAM FACEBOOK WALIWAZIDI MAARIFA TEAM MEDIA NA KUJIPATIA GOAL DAKIKA YA 80 NA MFUNGAJI AKIWA NI ADAM ARTETA na kufanya Matokeo yawe Facebook 1- 0 Media hadi Mpira Unaisha. WASANII KATIKA STAGE. Baada Ya mpira kuisha wadau waliokuja Ilikuwa mida kuburudika Na baadhi ya Wasanii mbali mbali, wasanii kama YOUNG TUSSO, COX DAWA YAO, COUNTRY BOY, BAGHDAD, STEVE SNIPER NA CANDY CALFONIA na wasani wengi ambao wali perform na kufanya watu wafurahi zaidi. BAADA YA SHOW HIYO KIONGOZI ALIPITA MBELE NA KUTANGAZA KILE KILICHOPATIKANA, PAMOJA NA MICHANGO YA HAPA NA PALE KIASI CHA SHILINGI 202,000. HATIMAE TULIFIKA TAMATI YA TAMASHA. TAREHE 6/7/2013 KUTAKUA NA MKUTANO MWINGINE IKIWA NI KWA AJILI YA KUJADILI CHANGAMOTO NA JUU YA UONGOZI NA MIKAKATI MINGINE....! NYOTE MNAKARIBISHWA AHSANTENI SANA. #Cable105.
Posted on: Mon, 01 Jul 2013 07:55:08 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015