Tumsifu Yesu Kristo! Ni Jumapili ya 33 ya mwaka wa kanisa! Karibu - TopicsExpress



          

Tumsifu Yesu Kristo! Ni Jumapili ya 33 ya mwaka wa kanisa! Karibu katika MAWIYO YA SIFA ,Mbarikiwa Jenny hapa! ”Bwana anakuja awahukumu mataifa kwa haki.” Masomo: Malaki 3:19-20; 2 Thesalonika 3:7-12; Luka. 21:5-19 Masomo yatualika kuishi maisha ya imani yetu tukiwa tayari kwa ujio wa Bwana wakati wowote. Vilevile tufahamu ya kwamba wakati tulio njiani kuelekea mbinguni,ni safari ambayo imejaa upinzani tele wa imani katika Bwana,hivyo tuwe tayari kuyapokea mateso wakati wote kwa matumaini. Hivi niulize Yesu anatuonya “ Muwe waangalifu, msije mkadanganyike”, je ni vipi tutaweza kuwa waangalifu? leo washiriki Ibada ya Misa wapi na saa ngapi?!
Posted on: Sun, 17 Nov 2013 02:51:53 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015