COCOSPORTS USIKU HUU: JUMAPILI, 06.10.2013: (Saa 3 kamili usiku - TopicsExpress



          

COCOSPORTS USIKU HUU: JUMAPILI, 06.10.2013: (Saa 3 kamili usiku huu). BAO za Kipindi cha Kwanza za Mrisho Ngassa, Dakika ya 5, na Didier Kavumbagu, Dakika ya 24, zimewapa Mabingwa Watetezi Yanga ushindi wa Bao 2-0 walipocheza na Mtibwa Sugar katika Mechi ya Ligi Kuu Vodacom iliyochezwa leo Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam. Pambano la Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya wenyeji Ruvu Shooting na Simba lililochezwa jana (Oktoba 5 mwaka huu) katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 75,692,000. BAO 3 za Kipindi cha Pili zimewapa West Ham ushindi wao wa kwanza Uwanjani White Hart Lane tangu Mwaka 1999 walipoitwanga Tottenham 3-0 katika Mechi ya Ligi Kuu England. LEO Mchana Straika hatari wa Atletico Madrid, Diego Simeone, alikosa kufunga Penati lakini baadae akapiga Bao 2 na kuipa Timu yake ushindi wa 2-1 walipocheza na Celta Vigo kwenye Mechi ya La Liga. Goli za mwishoni za Eden Hazard na Willian, wote wakitokea Benchi, zimewapa Chelsea ushindi wa kwanza wa Ugenini kwenye Ligi Kuu England Msimu huu walipoichapa Norwich Bao 3-1.
Posted on: Sun, 06 Oct 2013 17:51:30 +0000

Trending Topics




© 2015