HABARI KWA UFUPI:: MCHANA:: Mwenyekiti wa Umoja wa Maskauti - TopicsExpress



          

HABARI KWA UFUPI:: MCHANA:: Mwenyekiti wa Umoja wa Maskauti Wabunge nchini Abdulkarim Shah amechaguliwa kuwa Mweka hazina Mkuu wa Umoja wa Wabunge Maskauti duniani kwenye Mkutano Mkuu wa Umoja huo uliofanyika kuanzia Novemba sita hadi Nane mjini Tokyo Japan. Mbali na nafasi hiyo nyeti, bwana Shah ambaye pia ni Mbunge wa Mafia amechaguliwa kuwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Umoja wa Maskauti Wabunge Ulimwenguni. Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kurejea nchini akitokea kwenye Mkutano huo, bwana Shah amewashukuru wajumbe wa Mkutano huo kwa kumchagua kwenye nafasi hizo muhimu duniani na kwamba ushindi huo ni zawadi kwa watanzania wote. Kwenye Mkutano huo Tanzania iliwakilishwa na Wabunge watano maskauti.
Posted on: Wed, 13 Nov 2013 09:16:19 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015