UCHAGUZI WA MADIWANI ARUSHA NEC WANAHENYA: Taarifa ambazo - TopicsExpress



          

UCHAGUZI WA MADIWANI ARUSHA NEC WANAHENYA: Taarifa ambazo nimezipata jioni ya leo na za kuaminika kabisa zinaeleza kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Jaji Damiani Lubuva yuko Jijini Arusha na maafisa kadhaa wa Tume hiyo kwa ajili ya kushughulikia maswala ua Uchaguzi wa Madiwani kwa Kata nne za Jijini hapa ambao uliahirishwa mara mbili kufuatia shambulio la bomu na risasi kwenye mkutano wa kufunga kampeni za CHADEMA kiashi cha kupelekea vifo vya raia wa Tanzania wanne na zaidi ya 70 kujeruhiwa, miongoni mwao akiwemo Judith Mushi aliekuwa Katibu wa CHADEMA Kata ya Sokoni 1 aliyefariki papo hapo. Utakumbuka kuwa miongoni mwa majeruhi ambao walikimbizwa ICU kabla ya kupata nafuu ni pamoja na Katibu wa Mbunge wa Arusha Mjini Bw Gabriel Kivuyo na Mwenyekiti wa CHADEMA Kata ya Sombetini Ndg Madava.. wengine walikuwa watoto ndugu ambao walihamishiwa Nairobi. Kimsingi taarifa za jioni hii zinaeleza wazi kuwa Mwenyekiti huyo wa NEC, Jaji Lubuva ameomba kukutana na viongozi wa CHADEMA kesho saa tisa mchana kwa ajili ya kuzungumza muafaka wa Uchaguzi huo wa marejeo uliopangwa kufanyika tarehe 14 Julai 2013. NYEPESI ZILIZOVUJA Wakati taarifa za kikao cha jaji Lubuva na CHADEMA zikishindwa kueleza sababu hasa za kikao na maswala ya kujadiliwa, vyanzo binafsi vilivyoko ndani ya NEC vimedokeza kuwa kuna maswala yafuatayo ndio yaliyomsukuma Jaji Lubuva kutaka kufanya mazungumzo na CHADEMA. 1. Imefahamika kuwa Jaji Lubuva na Tume yake ya Uchaguzi wamedai (labda kwa shinikizo) kuwa hawawaamini Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ambao mara nyingi huwa ni walimu na watumishi wengine. Wamepanga kupeleka Arusha watu wao wengine wapya ambao wao wanawaamini zaidi. Sababu kubwa wanadai eti wasimamizi hao ni watu wa CHADEMA. (Nicheke kidogo.. te te teh! Naona hapa hofu umewatanda mpaka vichwani na hii inathibitisha utawala wa CHADEMA Arusha kwamba kila mtu utakaemchagua kufanya jambo unaona ni mtu wa CHADEMA...s). Mtanzania mwenzangu tuujiulize hofu hii ya nini wakati wananchi ndio wenye maamuzi? Je, kuna uhusiano wowote na tukio la bomu na haya yanayoendelea sasa?? Huu ni Uchaguzi wa Udiwani tu shida nmana hii, ungekuwa wa Urais hali ingekuwaje?? 2. Imefahamika kuwa Jaji Lubuva ameamua kusimamia mwenyewe Uchaguzi huo sambamba na watu wake hao wanaoaminika. Kumbuka hizi ni zile zilizovuja nje ya taarifa rasmi ya NEC CHADEMA KUDAI HAKI YA KUFANYA KAMPENI Taarifa nyingine pia na za kuaminika kuhusiana na uchaguzi huo zinaeleza teana kuwa CHADEMA kwa upande wao wanasubiria hicho kikao na yatakayojadiliwa lakini wao kwa upande wao wamejipanga kutumia nafasi hiyo kushinikiza marufuku ya kufanya kampeni iondolewe ili kampeni zifanyike. CHADEMA wanasema zuio la mikusanyiko kwa kigezo cha hali ya hatari hazima mashiko kwasababu baada ya bomu la awali la Olasiti Kanisani bado waumini waliendelea kuhudhuria Ibada zao, kwa hiyo bomu la kupigwa CHADEMA haliwezi kuwa na mazingira tofauti na lile la kanisani. Tutazidi kuhabarishana kwa kadiri taarifa sahihi na za kweli zitakavyokuwa zinapatikana
Posted on: Tue, 02 Jul 2013 20:41:52 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015