WACHEZAJI wa TAIFA STARS leo wanaingia katika uwanja wa NAMBOOLE - TopicsExpress



          

WACHEZAJI wa TAIFA STARS leo wanaingia katika uwanja wa NAMBOOLE nchini UGANDA kucheza na THE CRANES katika mchezo wa kufa ama kupona. Mchezo huo ni wa mwisho kwa timu hizo ambazo zinatafuta tiketi ya kucheza fainali za mashindano ya wachezaji wanaocheza soka la ndani ya CHAN. Kocha KIM PAULSEN amewaelekeza wachezaji wa TAIFA STARS kucheza kwa kushambulia muda mwingi ili waweze kufikia azma ya kucheza fainali hizo zitakazochezwa mwakani nchini AFRIKA KUSINI. Katika mchezo wa awali uliochezwa wiki mbili zilizopita TAIFA STARS ilichapwa goli MOJA kwa BILA na THE CRANES na hivyo kutakiwa kupata ushindi wa zaidi ya magoli MAWILI kwa BILA ili iweze kusonga mbele na mashindano ya CHAN. Hii ni fursa ya mwisho kwa TAIFA STARS kwani ina mchezo mmoja wa kukamilisha ratiba wa kombe la dunia dhidi ya GAMBIA utakaochezwa mwezi Septemba. Mchezo huo utaanza saa kumi jioni kwa saa za Afrika mashariki na utachezeshwa na mwamuzi kutoka MADAGASCA KANOSO ABDUL OHABEE. TAIFA STARS jana jioni imefanya mazoezi katika uwanja wa NAMBOOLE tayari kwa mchezo huo ambao TBC ONE utakuletea moja kwa moja mchezo huo kutoka nchini UGANDA. == == = = Chama cha walimu wa Mchezo wa mpira wa miguu,mkoani Mbeya TAFCA kimetangaza kuwafungia walimu ambaoo hawajalipia ada ya mwaka huu,kwamba hawataruhusiwa kufundisha soka katika vilabu wanavyofundisha hivi sasa. Katibu mkuu wa Chama hicho mkoani Mbeya THOMASI KASOMBWE amezungumza na waandishi wa habari na kutishia kutotoa vitambulisho vya kufundisha soka hadi kuwa na leseni stahili inayotolewa na TAFCA. Kwa taarifa zaidi na Hosea Cheyo == == = == == Bingwa mara sita wa riadha katika mashindano ya OLYMPIC USAIN BOLT jana ameendeleza ubabe wake katika mbio za mita 100 za michezo ya kuadhimisha mwaka mmoja wa OLYMPIC yaliyofanyika LONDON kwenye viwanja vya OLYMPIC Mwaka mmoja baada ya mashindano ya OLYMPIC kufanyika LONDON mwaka 2012 BOLT amekimbia sekunde 9.85 kwenye mashindano hayo hapo jana. Mwingereza JAMES DASALU alijiondoa kwenye kinyang’anyiro hicho kutokana na kupata majeraha. BOLT alianza taratibu lakini bingwa huyo wa OLYMPIC aliwashinda wapinzani wake kwenye hatua za mwisho MICHAEL RODGERS aliyekamata nafasi ya pili. NESTA CARTER wa JAMAICA yeye alikamata nafasi ya tatu akitumia muda wa sekunde 9.99 wakati DWAIN CHAMBERS mwingereza pekee aliyekua amesalia kwenye mbio hizo baada ya DASALU kujitoa alikamata nafasi ya tano kwa kutumia muda wa sekunde 10.10. BOLT ambaye sasa atatazamia kurejesha ubingwa wa dunia mwezi katika mashindano yatakayofanyika MOSCOW mwezi ujao amefurahishwa na kiwango alichokionesha jana mbele ya mashabiki ELFU SITINI. == = == == = Tukiangazia mashindano ya LANGALANGA hapo jana dereva wa RED BULL SEBASTIAN VETTEL alitawala mashindano ya majaribio ya HUNGARIAN GRAND PRIX Bingwa huyo wa dunia wa mashindano ya FORMULA ONE alimzidi dereva mwenzake MARK WEBBER BILA shida yoyote katika raundi zote. Dereva wa LOTUS ROMAIN GROSJEAN alikamata nafasi ya tatu akiwazidi FERNANDO ALONSON na FELIPE MASSA wa timu ya FERRARI pamoja na dereva wa MERCEDES LEWIS HAMILTON na NICO ROSBERG. KIMI RAIKONEN wa LOTUS ambaye anafukuzia ubingwa wa dunia alikimata nafasi ya nane baada ya kuzidiwa na dereva wa MCLAREN JENSON BUTTON. VETTEL aliwazidi madereva wa timu ya FORCE INDIA ADRIAN SUTIL na PAUL DI RESTA. = === == Katika masuala ya usajili kwenye soka klabu ya MANCHESTER UNITED jana imepata habari mbaya baada ya klabu ya BARCELONA kuendelea kusisitiza kuwa kiungo wao CESC FABREGAS hatouzwa kwa gharama yoyote. Makamu mwenyekiti wa klabu hiyo JOSEP MARIA BARTOMEU amesema hayo jana kuwa CESC hatouzwa kwa gharama yoyote. Siku ya Alhamisi meneja wa UNITED DAVID MOYES alisema kuwa mazungumzo kwa ajili ya dili la kumsajili FABREGAS yanaendelea lakini jana klabu hiyo ya LA LIGA imesema kuwa hakuna offer itakayokubaliwa kwa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26. BARTOMEU amesema kuwa nia ya UNITED kutaka kumsajili CESC iko wazi kwa kuwa ni mchezaji mzuri lakini nia hiyo haiwasumbui wao BARCELONA. Makamu huyo wa mwenyekiti akaendelea kusema kuwa haitojalisha kiasi gani watatoa kwa kiungo huyo kwa kuwa hawatomuuza. Mabingwa wa ligi ya ENGLAND wameshindwa na offer mbili walizotoa kwa BARCA huku ofa ya mwisho ikiripotiwa kuwa pauni milioni 30 na maongezo. Naye meneja mpya wa klabu hiyo GERALDO TATA MARTINO akaendeleza msimamo wa klabu hiyo kwa kusema kuwa kwa kuwa klabu imekataa ofa mbili za CESC basi yeye atakataa ofa ya tatu itakayokuja kwa ajili ya kiungo huyo. = = == = = == = Wakati huohuo timu hiyo ya MANCHESTER UNITED jana imeambulia sare ya bao mbili kwa mbili shukrani kwa WILFRED ZAHA aliyefunga bao la kusawazisha kwenye dakika za majeruhi. KENYU NUGIMOTO alianza kuipatia timu yake ya CEREZO OSAKA bao la kuongoza kwenye dakika ya 33 ya mchezo bao ambalo lilidumu hadi timu hizo zinakwenda mapumziko. Katika kipindi cha pili SHINJI KAGAWA ambaye ni mzawa wa JAPAN aliisawazishia UNITED akiunganisha vizuri krosi ya mkongwe RYAN GIGGS kwenye dakika ya 54. UNITED ilipata nafasi ya kusawazisha lakini penati iliyopigwa na SHINJI KAGAWA iliokolewa na kipa wa CEREZO. CEREZO OSAKA walizidi kuweka ngumu kwa MANCHESTER kwani kwenye dakika ya 64 shuti kali lililokwenda moja kwa moja wavuni lilipigwa na TAKUMI MINAMINO. Lakini kwenye dakika ya 91 WILFRED ZAHA kwa mara ya kwanza aliingia kwenye orodha ya wafungaji wa mabao wa UNITED kwa mwaka huu kwenye michezo ya kujipima nguvu kwa kuipatia UNITED bao la pili na la kusawazisha. UNITED imeshacheza michezo minne ambapo imefungwa michezo miwili na kushinda mmoja na kutoka sare mmoja hapo jana. == ===== ARSENAL jana imemaliza ziara yake barani ASIA kwa ushindi wa bao mbili kwa moja katika dhidi ya URAWA DIAMONDS ya JAPAN ukiwa ni ushindi wa nne katika michezo minne iliyocheza timu hiyo. Katika kipindi cha kwanza timu hizo mbili zilichoshana nguvu baada ya kumaliza kipindi hicho pasipo kufungana. LUKAS PODOLSKI ambaye aliingia kipindi cha pili alianza kuipatia ARSENAL bao la kuongoza kwenye dakika ya 49. Aidha URAWA walifanikiwa kusawasiaha bao hilo kwenye dakika ya 59 kupitia kwa YUKI ABE. THE GUNNERS ilijipatia bao la ushindi kupitia kwa mshambuliaji mwingine aliyeingia kipindi cha pili CHUBA AKPOM aliyetumia vizuri makosa ya mlinzi wa URAWA DIAMONDS ya kurudisha mpira vibaya kwa kipa wake kwenye dakika ya 83. THE GUNNERS sasa watarejea nyumbani kwa ajili ya michuano ya kombe la EMIRATES yatakayoanza wiki ijayo ambapo watakutana na NAPOLI na GALATASARY. = == === =
Posted on: Sat, 27 Jul 2013 04:49:04 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015