“WOTE: Salaam zako zimenifikia oo, ninashukuru kwa kunikumbuka, - TopicsExpress



          

“WOTE: Salaam zako zimenifikia oo, ninashukuru kwa kunikumbuka, yaliyonipata si mataatizo oo ni mabadiliko ya maisha. Misukosuko ni jambo la kawaida oo ukiwa bado hai matatizo hutoyakiimbiaa (mama) . Mfano ni yaliyomkuta nabii Yesu, kusalitiwa na Yudaa Skarioot. Duniani tu uwanja wa kupita. ********************************** WOTE: Umuonaye mwema wako aweza kuwa hasidi,umzaniaye mbaya kumbe ndiye wa kukuokoaa(matarumbeta) kiumbe habebeki (matarumbeta) SHAABAN DEDE: (Kwa hisia kali)Huwezi kupendwa na woteee au kuchukiwa na wote duniani. Huwezi kupendwa na wote Dede au kuchukiwa na wote ulimwenguni. Fitina za nini ubaya wa nini, chuki ya nini ubaya wa nini, uzushi wa nini ipi faida yake, uzushi wa nini ipi faida yake. Riziki yaangu huwezi chukua wewe, riziki ya mtu huwezi wekea zege mbinguni ,riziki yangu haiwekewi pazia. Hata Yesu Kristu alisalitiwa sembuse mimi Deede. WOTE: Umuonaye mwema wako aweza kuwa hasidi,umzaniaye mbaya kumbe ndiye wa kukuokoaa(matarumbeta) kiumbe habebeki (matarumbeta na sebene lenye solo lililopigwa kwa hisia kali kama yalivyokuwa maudhui ya wimbo huo)” Huu ni wimbo wa Bimalee, utunzi wa mwaka 1990 wa mwimbaji Shaaban Dede. Ulikuwa wimbo ulioujibu wimbo mwingine wa bendi hiyo wa mwaka 1988 ulioitwa Magombeka ulioongozwa kuimbwa na Athumani Momba (marehemu) ulioelezea barua aliyotumiwa mtoto (Dede) na wazazi wake(wanamuziki wa Bimalee) kumtaka arudi nyumbani (Bimalee) baada ya kupata matatizo huko mjini(JUWATA Jazz) alikokuwa akiishi wakati huo. Utunzi huu wa 1988 ulifuatia JUWATA Jazz kumsimamisha kazi Dede kwa kwenda kutazama mechi ya Simba na Sigara, iliyomalizika kwa suluhu, badala ya kwenda kazini kwenye muziki wa Jumapili ilipochezwa mechi hiyo. Muziki huo ulianza saa 10 jioni hapo Amana kama ulivyokuwa utaratibu wa kkila Jumapili. Dede ni Simba wa kupitiliza. HOJA ZANGU: 1. Dede ni mmoja wa watunzi mahiri wa misemo ya kuvutia na nasaha za nguvu kwenye tunzi zake za kila aina ya maudhu-mapenzi, maonyo,visa, mafunzo nk- kama alivyokuwa Joseph Mulenga (marehemu) 2. Tunzi za mashairi mazito kama hiyo ya 1990 zimeenda wapi leo wakati kina Dede wapo? 3. Radio zetu zina vipindi vingi vya kurusha muziki wa dansi wa miaka ya nyuma kwa kuweka mpaka wa miaka ya mwisho kuja miaka hii. Kama hilo ni lazima basi waongeze vipindi ili kipatikane cha muziki wa kufikia miaka ya 2000 ili tuzisikie radioni NA HIZI NAZO. 4. Utaratibu huu wa kibaguzi wa radio zetu unafanya nyimbo kama Kisa cha Mpemba, Jirani, Fainali Uzeeni, Chuki Binafsi na nyingine (za Twanga), Tunda Special, Chande na nyingine (za Tamtam), Mtaji wa masikini, Narudi nyumbani, Elimu ya mjinga, Mnyonge mnyongeni na nyingine(za ToT Plus) ZISUBIRI ZIWE ZILIPENDWA NDIPO ZISIKIKE TENA REDIONI! Non sense!
Posted on: Sat, 27 Jul 2013 08:48:21 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015