katika sports leo utasikia mengi lakini ni pamoja na KIKOSI cha - TopicsExpress



          

katika sports leo utasikia mengi lakini ni pamoja na KIKOSI cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, chini yake kocha wake, Mkuu Kim Poulsen kinatarajiwa kuingia kambini leo, katika hoteli ya Accommondia, Dar es Salaam kujiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Gambia itakayochezwa Septemba 7 mwaka huu nchini humo. Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kampuni ya Azam Media leo (Agosti 30 mwaka huu) wamesaini mkataba wa haki za kipekee za televisheni (exclusive rights) utakaoiwezesha Azam TV kuonesha mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL). MSIMU uliopita walipokutana kwenye Uwanja wa Emirates na wana fainali ya Ligi ya Mabingwa, Oktoba 22, matokeo yalikuwa Arsenal 0 Borussia Dortmund 0. MABINGWA mara saba wa Ulaya, AC Milan, waliotolewa na Barcelona katika Ligi ya Mabingwa misimu miwili iliyopita, wamepangwa kundi moja na vigogo hao wa Katalunya katika hatua ya makundi msimu huu baada ya droo iliyopangwa jana. utakuwa nami RICHIE FLAVOUR KOCHA MCHEZAJI
Posted on: Fri, 30 Aug 2013 16:31:09 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015