HABARI KWA UFUPI:: JIONI:: Zoezi la Serikali kuwarejesha kwa - TopicsExpress



          

HABARI KWA UFUPI:: JIONI:: Zoezi la Serikali kuwarejesha kwa hiari makwao wahamiaji haramu lililoanza kutekelezwa mwanzoni mwa mwezi huu kwenye mikoa ya Kagera, Kigoma na Geita limefanikisha kuwaondoa wahamiaji haramu elfu kumi mia sita sabini na wawili (10,672). Wahamiaji haramu waliorejea makwao pamoja na mali zao ni kutoka mataifa ya Rwanda, Burundi, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Dokta Emanuel Nchimbi amewataka viongozi wa vijiji nchini kuacha kuwasaidia wahamiaji haramu kupata maeneo ya kuishi, na kutoa onyo watakaobainika watafikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Posted on: Tue, 20 Aug 2013 13:29:55 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015