Hivi kweli ina leta maana akilini serikali moja kuwa na katiba - TopicsExpress



          

Hivi kweli ina leta maana akilini serikali moja kuwa na katiba tatu tofauti? (Rejea rasimu ya katiba 2013) Ibara ya ""8.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Katiba za Washirika wa Muungano kwa mambo yasiyo ya Muungano, Katiba hii itakuwa sheria kuu katika Jamhuri ya Muungano."" Je, hii ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania au Shirkisho la Tanzania? yaani Tanganyika na Zanzibar? kwani huwezi sema una Jamhuri ya Muungano angali bado ukakiri una nchi mbili tofauti ambazo zinazaa nchi nyingine na kupata nchi tatu tena zenye katiba kila moja (Rejea rasimu ya katiba 2013) Ibara ya ""57.-(1) Jamhuri ya Muungano itakuwa na muundo wa shirikisho lenye serikali tatu ambazo ni: (a) Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; (b) Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar; na (c) Serikali ya Tanzania Bara. (2) Shughuli za Jamhuri ya Muungano zitatekelezwa na kusimamiwa"" Je, rasimu inaposhindwa kutambua raslimali kama sehemu ya muungano lkn bado watu wapo kwenye sehemu ya muungano kikazi, JE watu siyo rasilimali?, au RASILIMALI WATIU KWA SASA TANZANI HAITAMBULIKI? watu wenye COMMUNITY DEVELOPMENT SKILLS NIPENI JIBU.
Posted on: Tue, 09 Jul 2013 21:43:28 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015